Abiria 900 ajali ya treni Tabora warudishwa makwao

Thursday June 23 2022
tabolaapiic
By Robert Kakwesi

Tabora.   Abiria wapatao 900 waliopata ajali katika treni ya abiria iliyotokea Kigoma, katika eneo la Malolo mjini Tabora, wamesafirishwa kwenda makwao kwa kutumia mabasi saba na treni ya abiria kutoka Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian amesema abiria hao wamesafirishwa usiku kuendelea na safari baada ya kupata ajali jana asubuhi.

Ameeleza majeruhi zaidi ya mia moja, wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao ameeleza kuwa waliopewa kipaumbele katika usafiri ni wanawake, wazee na watoto.

Ajali hiyo imetokea jana asubuhi katika eneo la Malolo, umbali wa km 10 kutoka stesheni ya Tabora.

Advertisement