Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afariki baada ya kukanyagwa na tembo

Afariki baada ya kukanyagwa na tembo

Muktasari:

Dayness Josephat (58) mkazi wa kata ya Maore Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro amefariki baada ya kukanyagwa na tembo wakati akienda shambani kwake.


Same. Dayness Josephat (58) mkazi wa kata ya Maore Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro amefariki baada ya kukanyagwa na tembo wakati akienda shambani kwake.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Igoma, Julius Mtegwa amethibitisha kutokea kwa tukio leo Jumatano Mei 26, 2021 saa 2 asubuhi.

"Hili tukio limetokea asubuhi leo wakati huyu mama na wenzake wakienda shambani, walikuwa watatu lakini wawili walifanikiwa kukimbia. Tembo amemrarua kila mahali hadi utumbo wake wote umetoka nje," amesema Mtegwa

Mei 23, 2021 naibu  Waziri wa Maliasili na Utalii, Marry Masanja alipofanya ziara wilayani Same na Mwanga alisema wizara hiyo imeweka mkakati wa namna ya kudhibiti tembo kutoingia kwenye makazi ya watu ikiwa ni pamoja na kuweka mizinga ya nyuki kwenye maeneo yote yalizozunguka hifadhi pamoja na kupanda miti.