Aika wa Navy Kenzo aeleza sababu kumuita mwanaye Jamaika

Muktasari:

Aika, mwanamuziki wa kundi la kizazi kipya la  Navy Kenzo linaloundwa na yeye pamoja na Nahreel, ametaja sababu za kumuita mwanaye Jamaika.

Dar es Salaam. Aika, mwanamuziki wa kundi la kizazi kipya la  Navy Kenzo linaloundwa na yeye pamoja na Nahreel, ametaja sababu za kumuita mwanaye Jamaika.

Akizungumza na Mwananchi jana Jumamosi Julai 27, 2019, Aika amesema mtoto wao huyo wa pili na mpenzi wake Nahreel  amepewa jina hilo kutokana na  maneno mawili ya Jamila na Aika yaliyozaa Jamaika.

Aika amesema Jamila ni jina la mama yake mzazi, kwamba waliamua kuyaunganisha na kumuita mtoto wao.

“Imekuwa faraja kwa mtoto wetu wa kwanza maana sasa amepata mdogo wake na wanaweza kucheza pamoja,” amesema Aika.