Airtel Africa yatangaza matokeo ya kifedha na kiutendaji kwa mwaka Machi 31, 2025

Dar es Salaam. Mtandao wa Airtel Africa umetangaza matokeoya kiutendaji na kifedha kwa mwaka ulioishia Machi 31, 2025, ikiashiria mafanikio ya mkakati wake unaolenga ukuaji wa kidijitali, ujumuishaji wa kifedha, na upanuzi wa mtandao katikamasoko yake 14 barani Afrika.
Katika taarifa iliyotolewa imeonesha Idadi ya wateja wote imeongezeka kwa 8.7asilimia na kufikia 166.1milioni, huku matumizi ya simu janja yakiongezeka kwa 4.3asilimia hadi kufikia 44.8 asilimia ya wateja wote.
Pia imeeleza ongezeko la wateja wa huduma za data kwa 14.1asilimia hadi 73.4milioni, huku matumizi ya wastani ya data kwa kila mteja yakiongezeka kwa 30.4asilimia hadi kufikia GB 7.0.
Watumiaji wa Airtel Money wameongezeka kwa 17.3asilimia hadi kufikia 44.6milioni, na thamani ya miamala ya kila mwaka ikifikia dola bilioni 145, ikiwa ni ongezeko la 34 asilimia kwa robo ya nne pekee.
Airtel imepanua mtandao wake kwa kufungua vituo vipya 2,583 na kusambaza zaidi ya 3,300 kilomita za nyaya za fibre, ili kuongeza uwezo wa kusafirisha data.
Katika utendaji wa kifedha taarifa imeeleza mapato yamefikia dola za Kimarekani 4.955bilioni, yakiwa yameongezeka kwa 21.1asilimia kwa kiwango thabiti cha fedha.
Mapato ya huduma za simu yameongezeka kwa 19.6 asilimia, yakichochewa na ongezeko la 30.5asilimia kwenye mapato ya data.
Mapato ya huduma za kifedha kwa njia ya simu yaliongezeka kwa 29.9ailimia. Faida kabla ya kodi (EBITDA) ilifikia dola 2,304milioni, na faida baada ya kodi imepanda hadi dola 328milioni kutoka hasara ya dola milioni 89 mwaka uliopita. Pia faida kwa kila hisa (EPS) ilikuwa senti 6.0, ikilinganishwa na -4.4 senti mwaka uliopita.
Usimamizi wa mitaji na madeni,uwekezaji wa mtaji (Capex) ulikuwa dola 670milioni, chini ya makadirio, huku Airtel ikitarajia kuwekeza kati ya dola 725milioni hadi dola750milioni mwaka ujao.
Kampuni imelipa dola 702milioni za madeni ya fedha za kigeni, na sasa 93asilimia ya madeni ni ya sarafu za ndani.
Bodi ya Wakurugenzi imependekeza mgawo wa faida wa senti 3.9 kwa kila hisa, na hivyo kufanya jumla ya mgawo wa mwaka mzima kuwa senti 6.5, sawa na ongezeko la 9.2ailimia.
Akizungumza kufiatia taarifa hio Mkurugenzi Mtendaji Mkuu, Sunil Taldar, "Tumeripoti matokeo thabiti tena, tukionyesha mafanikio ya mkakati wetu wa kuwekeza katika mtandao, kuboresha majukwaa ya kidijitali, na kutoa huduma bora kwa wateja. Wateja wa simu janja wameongezeka kwa 20 asimilia hadi 74.4milioni, na matumizi ya data yamepanda kwa 47.5asimia. Airtel Money inaendelea kuimarisha ujumuishaji wa kifedha na thamani ya miamala imepanda kwa 32asilimia kwa mwaka. Tunaendelea na maandalizi ya kuorodhesha Airtel Money kwenye soko la hisa mwaka 2026, kulingana na hali ya soko."
Tunaendelea na maandalizi ya hatua ya kuuza hisa za Airtel Money kwa umma (IPO), tukibaki waangalifu na hali ya soko inavyoendelea. Tunatarajia tukio hilo kufanyika katika nusu ya kwanza ya mwaka wa kalenda 2026, endapo mazingira yatakuwa mazuri.
Tunashukuru kwa uthabiti wa sasa wa mazingira ya uendeshaji, lakini bado tunaangalia kwa makini maendeleo ya kimataifa ambayo yanaweza kuathiri biashara yetu. Tutaendelea kutekeleza mkakati wetu wa kubadilisha maisha ya wateja wetu na kusaidia ustawi wa kiuchumi katika masoko yetu.
Ningependa kuwashukuru wateja wetu, washirika, serikali, na wasimamizi kwa usaidizi wao, na wafanyakazi wetu kwa mchango wao usiochoka."