Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mahakama yasogeza mbele usikilizaji maombi ubunge wa Baba Levo

Muktasari:

  • Wapiga kura wanne wa Jimbo la Kigoma Mjini wamefungua kesi kupinga ushindi wa mbunge wa jimbo hilo, Baba Levo. Mahakama imeanza kusikiliza maombi madogo ya kuongezewa muda kuwasilisha maelezo ya mashahidi kabla ya kuingia kwenye ushahidi.



Kigoma. Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Kigoma imesogeza mbele usikilizaji wa maombi ya nyongeza ya muda wa kuwasilisha maelezo ya mashahidi wa walalamikaji katika kesi ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini, kutoka saa 6:00 mpaka saa 8:00 mchana wa leo Alhamisi, Juni 18, 2026.

Kesi hiyo ya uchaguzi namba 28949 ya Mwaka 2025 imefunguliwa na wananchi wanne, Johary Kabourou, Loum Mwitu, Pendo Kombolela na Luma Akilimali dhidi ya Tume Huru ya Uchaguzi, mbunge wa jimbo hilo, Clayton Revocatus Chipando, maarufu Baba Levo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Walalamikaji hao wanapinga ubunge wa Baba Levo aliyetangazwa kushinda kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akimzidi mpinzani wake mkubwa kutoka ACT-Wazalendo, mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Zitto Kabwe.

Kesi hiyo ilikuwa imepangwa kuanza kusikilizwa leo ushahidi wa walalamikaji, lakini walichelewa kuwasilisha mahakamani maelezo ya maandishi ya mashahidi wao, hivyo wakafungua maombi madogo wakiomba kuongezewa muda wa kuwasilisha maelezo hayo ya mashahidi.

Maombi hayo madogo yalikuwa yamepangwa kuanza kusikilizwa saa 5:00 asubuhi na kesi ya msingi ya usikilizwaji wa ushahidi ilikuwa umepangwa kuanza saa 6:00 mchana kutegemeana na uamuzi wa mahakama katika maombi hayo madogo.

Hata hivyo, mwanasheria mkuu wa ACT- Wazalendo, Wakili Omary Said Shaaban amesema baada ya kujadiliana na Jaji anayesikiliza kesi hiyo, Victoria Nongwa katika chemba yake, usikilizwaji wa maombi hayo madogo umesogezwa mbele mpaka saa 8: mchana.

"Hivyo kutokana na ratiba hiyo leo usikilizwaji wa ushahidi (kama maombi hayo madogo yatakubaliwa) hautafanyika," amesema Wakili Shaaban akitoa mrejesho kwa wafuasi wa chama hicho walifika mahakamani kusikiliza kesi hiyo, baada ya majadiliano na Jaji Nongwa.

Uamuzi wa maombi haya madogo ndio utatoa hatima ya usikilizwaji wa kesi ya msingi katika hatua ya ushahidi.

Hii inamaanisha kama mahakama katika uamuzi wake haitayakubali maombi hayo madogo, kesi hiyo itaondolewa mahakamani kwani bila kuwepo kwa maelezo ya mashahidi hao mahakamani, mashahidi hawawezi kutoa ushahidi, na hivyo hakutakuwa na kesi.

Katika kesi hiyo walalamikaji hao wanadai kuwa wanadai kuwa uchaguzi huo uligubikwa na kasoro nyingi.

Wanabainisha kasoro hizo kuwa ni pamoja na ukiukwaji wa taratibu, kanuni na Sheria za Uchaguzi, vitendo vya rushwa na udini vilivyooneshwa na mlalamikiwa wa pili, Baba Levo.

Hivyo wanaiomba mahakama hiyo pamoja na mambo mengine iamuru ufanyike upekuzi na uhesabuji upya wa karatasi za kupigia kura na kisha ibatilishe na kutengua uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa wakili wa walalamikaji hao, John Seka, wanatarajia kuwaita mashahidi wasiopungua 20 na kuwasilisha vielelezo mbalimbali.


Endelea kufuatilia Mwananchi