Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Akamatwa kwa kujiunganishia bomba la mafuta nyumbani kwake

Muktasari:

Samwel anashikiliwa kwa tuhuma za kutoboa na kujiunganishia bomba la mafuta la TPA

Dar es Salaam. Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wakishirikiana na Jeshi la Polisi wanamshikilia Samwel Kilang'ani(63) kwa tuhuma ya kutoboa bomba la mafuta ya dizeli mali ya TPA na  kujiunganishia hadi kwenye nyumba yake ambako ameweka mantanki makubwa ambayo ameyachimbia chini.

Msemaji wa TPA,  Janeth Ruzangi amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo huku polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ikiendelea kumshikilia kwa uchunguzi zaidi.