AKU yatoa mafunzo zana za kufundishia

Thursday June 23 2022
kiu
By Mwandishi Wetu

Morogoro. Chuo Kikuu cha Aga Khan (AKU- IED) kimetoa semina kwa walimu zaidi ya 50 katika Wilaya ya Turiani mkoani hapa kuhusu matumizi ya zana za gharama nafuu au zisizo na gharama katika kutoa stadi za kusoma na kuandika kwa wanafunzi.

Akizungumzia semina hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, mkuu wa chuo hicho Dk Jane Rarieya amesema ililenga kuonyesha na kukuza uwezo wa walimu juu ya zana na rasilimali ambazo zitawasaidia katika kutoa na kukuza umahiri kwa wanafunzi wao kwa mujibu wa.

"Mara nyingi unapowauliza walimu kwa nini wanafunzi hawafanyi vizuri katika kuhesabu, kusoma na kuandika watakuambia kuwa hawana rasilimali na vifaa vya kufunidshia, wakati kuna rasilimali nyingi karibu yao, kwa hiyo tulikuwa tunawaonyesha rasilimali hizo ili wazitumie," alisema.

Ofisa Elimu Taaluma wa Wilaya ya Mvomero, Gundelinda Chami alisema ujuzi huo ni muhimu sana kwa sababu unawaonyesha kwa vitendo walimu jinsi ya kutumia vitu vinavyowazunguka kwa matumizi ya kufundishia lakini pia kuwafundisha wanafunzi kuandaa zana hizo.

"Wengi wetu (walimu) tunafikiri zana za kutolea elimu ni zile tunazojitayarishia wenyewe au lazima tununue kwenye maduka lakini mafunzo yalitusaidia kutambua zana hizi kwenye maeneo yetu na pia kuwawezesha wanafunzi kujiandalia wenyewe," alisema

Fidelisi Thomas, mwalimu wa shule ya msingi Turiani B amesema warsha hiyo mmemkumbusha zaidi licha ya matumiz iya vifaa nafuu bali pia kuwashirikisha zaidi wanafunzi katika uwasilishaji na kuwaacha waeleze wanavyoelewa wenyewe.

Advertisement

Kwa mujibu wa viongozi wa AKU zaidi ya shule 91 zikiwemo 10 za Turiani na Mvomero zimefikiwa na mradi huu katika mikoa 8 ya Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Arusha, Mtwara, Singida, Manyara na Iringa.

Jumla ya vitabu 36,310 vikiwemo 500 kwenye warsha ya siku hiyo na zaidi ya 4,031 vimechangwa. Zaidi ya hayo, zaidi ya wanafunzi 72,800 na walimu 1,001 wamefikiwa mtawalia.

Advertisement