Alichokisema Waziri Lugola kuhusu wakimbizi wa Burundi kurejea nchini kwao

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola

Muktasari:

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema Serikali haitavumilia watu, mashirika yatakayokwamisha mchakato wa kuwarejesha wakimbizi wa Burundi kwao

Kigoma. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema Serikali haitavumilia watu, mashirika yatakayokwamisha mchakato wa kuwarejesha wakimbizi wa Burundi kwao.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Agosti 25, 2019 baada ya kutembelea kambi ya wakimbizi Nduta iliyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani na Maendeleo ya Vijiji wa Burundi, Pascal Barandagiye.

Akiwa katika kambi ya wakimbizi ya mpito ya Shirika la Ugawaji Ia Taifa (MNC), Lugola amesema  wapo wakimbizi wamerejeshwa makwao kwa hiari na bado wengine wanajiandikisha.

Amesema wakimbizi wa Burundi waliopo Tanzania wanalelewa vyema na sasa ni wakati wa kurejea nchini humo kwa kuwa kuna amani, atakayekwamisha hilo Serikali haitamuacha salama.

Kwa upande wake,  Barandagiye amesema Serikali ya Burundi ipo tayari kutekeleza makubaliano ya kuhakikisha wakimbizi wote wa nchi hiyo waliohifadhiwa kwenye kambi mbalimbali wanarejea kwao.