Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyekutwa mtupu chumbani kwa binti yake, akwama rufaa

Muktasari:

  • Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Tabora, imethibitisha kifungo cha miaka 30 jela kwa mkazi wa Kijiji cha Masagala, Kata ya Misha mkoani Tabora, baada ya kutupilia mbali rufaa yake ya kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kuzini na binti yake wa kumzaa aliyekuwa na miaka 13.

Arusha. Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Tabora, imethibitisha hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela alichokuwa amehukumiwa mkazi wa Kijiji cha Masagala, Kata ya Misha mkoani Tabora, baada ya kukutwa hatiani kwa kosa la kuzini (kumbaka) binti yake wa kumzaa aliyekuwa na umri wa miaka 13.

Wakati wa kesi ya msingi inasikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tabora, baba huyo (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili), ushahidi wa mkewe katika kesi hiyo ulidai kuwa alimkuta chumbani kwa binti huyo usiku wakiwa mtupu kama alivyozaliwa na alipoulizwa alidai alikuwa akifukuza panya.

Uamuzi uliothibitisha hukumu hiyo umetolewa Julai 24, 2026 na Jaji Martha Mpaze, aliyekuwa akisikiliza rufaa iliyokatwa na baba huyo ambapo aliitupilia mbali, akisema upande wa mashtaka ulithibitisha kosa hilo bila kuacha shaka yoyote ya msingi.

Jaji amesema baada ya kupitia upya ushahidi wote ikiwemo ushahidi wa mwathirika wa tukio hilo ulikuwa wa moja kwa moja, thabiti na wa kuaminika, huku ukiungwa mkono na ushahidi wa mama yake aliyemkuta mrufani akiwa mtupu chumbani kwa binti yao usiku.

Hata hivyo, maelezo hayo hayakumridhisha mama huyo, ndipo binti yao alipofichua kuwa siku moja kabla baba yake alikuwa amembaka na kumtishia asimwambie mtu yeyote.

Mahakama imeeleza kuwa tukio hilo lilifichuka baada ya mama wa mtoto kuamka usiku na kugundua mumewe hayupo kitandani na alipoenda chumbani kwa binti yao alimkuta na mtoto huyo wakiwa utupu.

Jaji alibainisha kuwa maelezo ya mrufani kwamba alikuwa akimfukuza panya hayakuwa ya kuaminika na hayakutoa maelezo ya kuridhisha kuhusu mazingira aliyokutwa nayo.

Amesema ingawa Mahakama ilibaini kuwa kulikuwa na kasoro kadhaa za kiutaratibu, ikiwemo kutokuwapo kwa ushahidi wa daktari na ushahidi wa shahidi mmoja kupokelewa bila kiapo, alisema kasoro hizo hazikuathiri msingi wa kesi kwa sababu ushahidi uliobaki ulitosha kuthibitisha kosa.

“Baada ya kutathmini upya ushahidi uliorekodiwa, naona upande wa mashtaka ulithibitisha vipengele vyote vya kosa la kujamiiana na mwanafamilia bila shaka yoyote, kwa sababu hizo, rufaa hii haina msingi na inatupiliwa mbali, hukumu na adhabu ya kifungo cha miaka 30 inathibitishwa,” amesema Jaji Mpaze.


Msingi wa kesi

Upande wa mashtaka uliiambia Mahakama ya Wilaya ya Tabora kuwa Julai 13, 2025, katika Kijiji cha Masagala, baba huyo alizini na binti yake wa kumzaa (jina limehifadhiwa), aliyekuwa na umri wa miaka 13.

Shahidi wa pili, ambaye ni mwathirika wa tukio hilo, alidai siku ya tukio alikuwa nyumbani yeye na baba yake, alidai baba yake alimfuata chumbani, akamvua nguo na kumbaka.

Alidai kupiga kelele kuomba msaada lakini hakuna aliyemsikia, huku baba yake akimtishia asimweleze mtu yeyote kuhusu tukio hilo.

Shahidi wa kwanza ambaye ni mama wa mtoto, alidai mahakamani kuwa usiku uliofuata alipoamka aligundua mumewe hakuwa kitandani na alipoenda chumbani kwa binti yao alimkuta mrufani na mtoto huyo wakiwa utupu.

Alidai alipomuuliza kwa nini alikuwa chumbani hapo, mrufani alidai alikuwa akimfukuza panya, maelezo hayo yalimtilia shaka, ndipo binti yao alipomweleza kuwa baba yake alikuwa amembaka siku moja kabla.

Alidai baada ya kupata taarifa hizo, alitoa taarifa kwa viongozi wa kijiji na ndugu wa familia, kabla ya suala hilo kuripotiwa polisi.

Mashahidi wengine wa mashtaka walieleza hatua zilizochukuliwa baada ya taarifa kutolewa, ikiwemo kukamatwa kwa mtuhumiwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, huku upande wa mashtaka ukisisitiza kuwa ushahidi wa mwathiriwa pamoja na mazingira ya tukio ulithibitisha kosa hilo bila kuacha shaka.

Suala hilo liliripotiwa kwa viongozi wa kijiji na baadaye polisi, hatua iliyosababisha kukamatwa kwa mtuhumiwa na kufikishwa Mahakama ya Wilaya ya Tabora, ambako alitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kuzini na binti yake kinyume cha kifungu cha 158(1) cha Kanuni ya Adhabu.


Rufaa

Kutokana na kutoridhishwa na adhabu hiyo alikata rufaa akiwa na sababu saba za rufaa ikiwemo Hakimu alikosea kumtia hatiani kwa kutegemea ushahidi wa mwathiriwa, akisema mtoto huyo hakuwa shahidi wa kuaminika kwa kuwa alitoa ushahidi bila uwepo wa Ofisa wa Ustawi wa Jamii kama inavyotakiwa na sheria.

Pia, alidai kulikuwa na tofauti katika ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, hususan kati ya mama wa mtoto na mwathiriwa kuhusu mazingira ya tukio, lakini Mahakama haikuzingatia dosari hizo pamoja na daktari aliyemfanyia uchunguzi mwathirika wa tukio hilo hakuitwa mahakamani kutoa ushahidi.

Sababu nyingine ilikuwa kwamba Mahakama ya Wilaya haikuzingatia ipasavyo utetezi wake kabla ya kumtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela.