Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyekutwa na kilo nne za majongoo bahari akiri shtaka

Majongoo bahari

Dar es Salaam. Raia wa China, Wei Zhang (54) amekiri kukutwa na  kukutwa na Jongoo bahari wenye uzito wa kilo 4.10,  ambao wapo hatarini kutoweka.

Zhang ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Kinondoni, amekiri shtaka lake leo Julai 6, 2023, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH).

Mshtakiwa huyo amekiri shtaka hilo muda mfupi baada ya kukumbusha shtaka lake na upande wa mashtaka.

Wakili Serikali, Tumaini Maingu akishirikiana na Cathbert Mbilingi, alimsomea upya hati ya mashtaka mbele ya hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa alikiri kukutwa na majongoo bahari na ndipo upande wa mashtaka walipoiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi wiki ijayo ili wawasilishe vielelezo na kumsomea maelezo.

“Mheshimiwa hakimu kwa kuwa mshtakiwa amekiri shtaka lake, tunaomba ahirisho fupi ili tuweze kulete vielelezo (majongoo bahari) mahakamani hapa na kumsomea maelezo yake,” amedai wakili Maingu.

Hakimu Shaidi amekubaliana na ombi la upande wa mashtaka na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 10, 2023, ambapo mshtakiwa atasomewa maelezo yake pamoja na hukumu.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti.

Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anakabiliwa kesi ya jina namba 113/2023.

Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2023 katika mtaa wa Kumbukumbu uliopo Kinondoni.

Siku hiyo ya tukio, mshtakiwa huku akijua jamii hiyo ya majongoo bahari ipo hatarini kutoweka, alikutwa akiwa na kilo 4.10 za majongoo bahari (Sea Cucumber) kinyume cha sheria.

Kwa mara  ya kwanza  mshtakiwa alifikishwa mahakamani hapo Juni 26, 2023 na kusomewa kesi hiyo.