Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyekuwa OCD Simanjiro afariki dunia ghafla

Aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara (OCD), marehemu Mathayo Mmary ambaye amefariki dunia ghafla kwa ugonjwa wa shinikizo la damu jana jioni alhamisi Juni 8 mwaka 2023.

Muktasari:

  • Mkuu huyo wa polisi wa wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara (OCD) Mathayo Mmary amefariki dunia kwa ugonjwa wa shinikizo la damu baada ya kuanguka ghafla akiwa saluni ya kunyoa nywele.

Simanjiro. Aliyekuwa Mkuu wa polisi wa wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, (OCD) Mathayo Mmary amefariki dunia ghafla kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dk Suleiman Serera ameyasema hayo mji mdogo wa Mirerani leo ijumaa Juni 9 mwaka 2023 kwenye ziara ya mkuu wa mkoa huo Queen Sendiga.

Dk Serera amesema OCD Mmary amefariki dunia ghafla jana Juni 8 mji mdogo wa Orkesumet baada ya kuanguka ghafla akiwa anaenda kunyoa nywele saluni.

"Baada ya kuanguka ghafla akakimbizwa hospitalini na kufariki dunia, tupo na majonzi pia ni juzi tuu hapa alipata taarifa ya uhamisho wa kwenda mkoa wa Singida hivyo alikuwa kwenye maandalizi ya kuaga," amesema Dk Serera.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ametoa pole kwa askari polisi wote na viongozi wa wilaya hiyo ya Simanjiro kwa msiba huo.

"Poleni sana kwa msiba askari polisi wote na viongozi wa Simanjiro kwani mmefanya kazi na aliyekuwa OCD wenu ambaye akapata uhamisho kwenda eneo jingine na kabla ya kuagana naye akafariki dunia ghafla," amesema Sendiga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, George Katabazi amesema mwili wa marehemu OCD Mmary utaagwa kesho jumamosi Juni 10 kwenye kituo cha polisi Mirerani.

Kamanda Katabazi amesema baada ya kuagwa mwili huo utapelekwa mji mdogo wa Boma ng'ombe, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, kwa taratibu nyingine za maziko.