Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amana za wateja zaipa rekodi KCB

Mwenyekiti wa Bodi Benki ya KCB-Tanzania, John Ulanga

Muktasari:

  • Amana za wateja wa KCB Tanzania, zimeiwezesha benki hiyo kuweka rekodi ya kufikia mali zenye thamani ya shilingi trilioni moja kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2022.

Dar es Salaam. Amana za wateja wa KCB Tanzania, zimeiwezesha benki hiyo kuweka rekodi ya kufikia mali zenye thamani ya shilingi trilioni moja kwa kipindi cha robo tatu ya mwaka 2022.

Rekodi hiyo ni kufuatia ongezeko la amana kwa asilimia 105 ndani ya kipindi cha miaka mitano, huku faida ya benki hiyo ikiongezeka kwa asilimia 182 hadi Sh22.4 bilioni kwa kipindi kama hicho.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 26 Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB-Tanzania, Cosmas Kimario wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya benki hiyo katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2022.

Amesema mafanikio ya benki hiyo imetokana na mikakati ya benki hiyo kukuza huduma na kuimarika kwa mazingira ya biashara nchini.

"Mikopo chechefu imeshuka kwa asilimia 17 kufikia asilimia tatu kiwango ambacho kinakubalika na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), tunatoa mikopo kwa kushauri wateja," amesema.

Pia Kimario amesema mafanikio hayo yamechangiwa na kasi ya wateja kutumia huduma za intaneti katika benki, miamala ya benki kupitia simu na njia POS ambazo zimeendelea kukoleza ufanisi wa huduma kwa wateja.

Mbali na hayo amesema mafanikio hayo yamechangiwa na namna walivyoboresha na kukuza rasilimali watu hatua iliyowawezesha kupunguza gharama za uendeshaji hadi asilimia hadi asilimia 49 kwa miaka mitano iliyopita.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCB, John Ulanga amesema benki hiyo ina mkakati wa kuongeza matawi matano ndani ya miaka miwili ijayo kwenye Mikoa ya Songwe,Geita na Kahama.