Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ambaka mama yake mzazi, amuua

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Agustino Senga.

Muktasari:

Inadaiwa kuwa mkazi huyo ambaye anaishi nyumba moja na mama yake alifanya tukio hilo akiwa amelewa baada ya kuvuta bangi na kurudi nyumbani ambapo alimkuta mama yake pia amelewa pombe za kienyeji.

Babati. Mkazi wa mtaa wa Wang'waray mjini Babati mkoani Manyara anashikiliwa na polisi akidaiwa kumbaka mama yake mzazi, kisha kumuua kwa kumchinja akitumia panga. 

 

Inadaiwa kuwa mkazi huyo ambaye anaishi nyumba moja na mama yake alifanya tukio hilo akiwa amelewa baada ya kuvuta bangi na kurudi nyumbani ambapo alimkuta mama yake pia amelewa pombe za kienyeji. 

 

Akizungumza  leo Juni 21 na Mwananchi, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Asia Ramadhani alisema mwanamke huyo alifariki dunia Juni  19 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake katika mtaa huo. 

 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Agustino Senga amesema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 51, alifariki dunia kwa kukatwa shingoni na kitu chenye ncha kali baada ya kubakwa. 

 

"Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kabla ya kufanyika kwa mazishi," amesema Kamanda Senga.