Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu azungumzia kupotea kwa watu

TAMKO LA MWANANCHI COMMUNICATIONS LIMITED KUPOTEA KWA MWANDISHI AZORY GWANDA

Muktasari:

Aman alikuwa akijibu maswali ya wanahabari leo Ijumaa, waliotaka kujua msimamo wake juu ya vitendo vilivyoanza kushamiri vya kutekwa na kupotea kwa watu nchini.

Moshi. Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi, Issac Aman amezungumzia hali ya kupotea kwa watu nchini, akisema kumficha mtu haimaanishi unaziba ukweli.

Askofu Aman alikuwa akijibu maswali ya wanahabari leo Ijumaa, waliotaka kujua msimamo wake juu ya vitendo vilivyoanza kushamiri vya kutekwa na kupotea kwa watu nchini.

Askofu Aman alienda mbali na kueleza kuwa kutoweka kwa watu sio ajali bali ni mipango ambayo isipofanyiwa kazi, nchi itakuwa inajidanganya ina amani kumbe sio.

Kauli ya Askofu huyo imekuja zikiwa zimepita siku 26 tangu kutoweka kwa mwandishi wa kampuni ya Mwananchi Communication Ltd (MCL) Wilaya ya Kibiti, Azory Gwanda.

MCL ni wachapishaji wa magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti na tayari wamepaza sauti zao wakitaka mwandishi huyo arejeshwe akiwa salama aendelee na majukumu yake.

Pia kauli ya kiongozi huyo, imekuja zikiwa zimepita siku 365 tangu kutoweka kwa Ben Saanane, aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Askofu alitoa kauli hiyo baada ya kubariki kanisa jipya la mtakatifu Yudathadei lililopo ndani ya Chuo Kikuu cha Katoliki cha Mwenge (Mwecau) nje kodo ya mji wa Moshi.

“Wau wanatowekaje? Watu wanapotea tu. Wananchi wanashangaa na hata watu wa nje watatushangaa. Watu wanapoteaje kutoka nyumbani? Alihoji na kuongeza;-

“Anaenda nyumbani anafuatiliwa huko halafu anachukuliwa kwenye gari na haonekani tena,” alisema Askofu Aman, mazingira ambayo ndio aliyotoweka mwanahabari Azory.

“Hiyo si ajali hiyo ni mipango ambayo tusipoifanyia kazi tutajidanganya kuwa tunakaa kwa amani. Hiyo sio amani. Hiyo ni cheche ya fujo kwenye nchi,” alisisitiza Askofu.