Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Askofu Rweyongeza: Ishi maisha yako, usishindane naya mwenzako

Askofu wa jimbo Katoliki la Kayanga Almachius Rweyongeza akiongoza ibada ya mkesha wa mwaka mpya 2023 na kuaga mwaka 2022 iliyofanyika katika kanisa kuu la mtakatifu Goerge lililopo makao makuu ya jimbo hilo Kayanga

Muktasari:

  • Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga, Almachius Rweyongeza amesema Watanzania waache kushindana na wenzao kwani kufanya hivyo watazalisha wivu hasi ambao hauleti maendeleo.

Karagwe. Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga, Almachius Rweyongeza amesema Watanzania waache kushindana na wenzao kwani kufanya hivyo watazalisha wivu hasi ambao hauleti maendeleo.

Askofu Rweyongeza ameyasema hayo katika ibada ya mkesha ya kuaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2023 iliyofanyika Kanisa Kuu la Mtakatifu Goerge lililopo makao makuu ya jimbo hilo.

"Katika kujilinganisha na mwenzako matokeo yake ni wivu hasi yaani wivu ambao hauleti maendeleo wa kumuharibia maendeleo yule mwenye nayo, matokeo yake unapojilinganisha na mwingine ni ushindani usiyo na tija au kuiga na kuibia majibu ya wengine bila kuzingatia kuwa kila binadamu amepewa mtihani wake wa kujibu," amemsema  

"Kila mtu amepewa swali ambalo haliwezi kujirudia kwa mtu mwingine toka kizazi cha Adamu na Eva hadi kiama. Hii inadhihirishwa hatufanani kila mtu ana umbo lake, ana sura yake, ana alama za vidole tofauti na za mwingine na amezaliwa mazingira tofauti na ya mwingine," amesema Askofu Rweyongeza

Amesema kila mtu na aupime mwenendo wake mwenyewe akiwa mwema basi anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine maana kila mmoja anao mzigo wake wa kubeba.

Katika mahubiri yake, ametolea mfano wa watu mashuhuri waliotangulia kuwa walikuwa na mkakati uliowahakikishia mafanikio yao na umoja wao na akatolea mfano wa Papa Mstaafu Benedict wa 16 ambaye ameaga dunia jana Jumamosi Desemba 31, 2022 na kuwa hao watu mashuhuri walijijua ni akina nani hawakuwa na muda wa kujiingiza kwenye mambo ya wengine.

"Mtafiti mmoja amesema ukijiingiza kwenye mambo ya wenzako hutapata muda wa kushughulikia ya kwako, yaani kuingia ndani ya moyo wako ukaangalia uwezo ambao Mungu amekujalia kukuletea amani, maendeleo na furaha ili usibaki kuhuzunika.

”Watu mashuhuri walitafuta muda kutafakari juu ya uwezo wao, vipaji vyao, vipawa vyao vilivyowatofautisha na wengine na wakatumia muda wao wakipiga msasa kukuza vipaji vyao, kila mmoja ana kipaji hivyo wavitumie katika kujiletea maendeleo yao wakimtanguliza mbele Mwenyezi Mungu.

Filomina Kakwesi, muumini katika kanisa hilo amesema mafundisho ya Askofu huyo yanawaanda kuendelea kumtumaini Mwenyezi Mungu na kuacha wivu usio na tija.

Naye Laurent Severin amesema, ujumbe wa Askofu Rweyongeza wa kila mmoja kushughulika na mambo yake bila kufuatilia ya wengine umemuingia akilini kwani mafalakano mengi yamekuwa yakitokana na wivu pengine wa kuzidiana uwezo wa kipato.