Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ataka mpango wa maendeleo usitenge mikoa duni


Muktasari:

  • Wabunge wameendelea kujadili na kushauri Serikali kuboresha mpango wa Maendeleo wa Taifa ili kutoacha nyuma baadhi ya maendeleo.

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Neema Lugangira ametaka Serikali ihakikishie Mpango wa Maendeleo ya Taifa uwe na sura ya kitaifa kwa kutoiacha nyuma mikoa yenye changamoto za kimaendeleo.

 Lugangira amesema hayo leo Jumatano Novemba 8, 2023 wakati akichangia kuhusu mpango huyo pamoja na mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2024/25.

Ametaka wakati Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo anahitimisha hoja yake, awaeleze ni namna gani atakahakikisha mpango huo utanufaisha maeneo yote nchini, huku akiutolea mfano Mkoa wa Kagera ambao amedai umeachwa nyuma.

“Ni muhimu kuhakikisha maendeleo yanatawanywa katika maeneo yote, katika kufanya hivyo, inabidi kuweka mipango thabiti ambayo itatafuta nyenzo na njia mbalimbali ambazo zitahakikisha mikoa ambayo iko katika hali ya umasikini, inainuliwa kwa kuchochea ukuaji wa uchumi,” amesema.

Amesema jambo hilo hata Rais Samia Suluhu Hassan ameshalisemea mara nyingi na kwamba anakumbuka katika ziara yake alivyokwenda katika Mkoa wa Kagera alisema mkoa huo kwa jiografia yake haupaswi kuwa mikoa inayoongoza kwa umasikini.

Amesema Rais Samia alielekeza kufanyika kwa tathimini mbalimbali na kuangalia jinsi ya kuhuisha pamoja na mikoa mingine katika jambo ambalo anadai mpango huo haujaeleza mikakati thabiti ya kuinua uchumi katika mikoa yenye hali ya umasikini.

Aidha amesema hajaona mipango dhabiti ya kuinua mkoa huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa soko la mazao ya kilimo, uvuvi na ufugaji.

Amesema pia mkoa huo hauna viwanda vya kutosha vya samaki, fedha za misaada kutoka wadau kutotawanywa katika maeneo yote, uwekezaji usioridhisha katika sekta ya afya, kukosekana kwa chuo kikuu ambapo wangeweza kupata wanafunzi kutoka Rwanda, Burundi na Uganda.

Amesema mkoa wa Kagera una kiasi kikubwa cha utapiamlo na udumavu lakini hakuna mradi wowote wa maendeleo ambao unawasaidia katika kupambana na udumavu.

“Hapa inaonyesha jinsi gani tunavyoweza kuhuisha malengo yetu maendeleo na mipango yetu ya maendeleo,” amesema.