Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Atupwa jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto wa miaka 13 Rombo

Muktasari:

  • Hukumu imetolewa baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 13, tukio ambalo linatajwa kutokea Machi 14, 2023.

Rombo. Mahakama ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, mkazi wa Kijiji cha Mbomai, wilayani humo, Ally Mbwambo (41) kwa kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 13.

Kesi hiyo ya ubakaji namba 14008/2023, ilifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Desemba 28, 2023, mbele ya Hakimu wa Wilaya hiyo, Innocent Nyella.

Inadaiwa Machi 14, 2023 mshitakiwa huyo kwa makusudi, alimbaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka 13 na kumsababishia maumivu makali.

Awali, akitoa hukumu hiyo jana Jumatano Agosti 7, 2024 Hakimu Nyella ameieleza mahakama hiyo wamejiridhisha na maelezo yaliyotolewa na mashahidi wa pande zote kwamba mshitakiwa huyo pasi na shaka alimbaka mtoto huyo.

Hata hivyo, Hakimu Nyella amesema mshitakiwa huyo atatakiwa kutumika adhabu ya kifungo hicho cha miaka 30 jela baada ya kukutwa na hatia hiyo.