Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Auawa kwa fumanizi, muuaji ajisalimisha polisi

Muktasari:

Mkazi wa kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Juvenal Claudi (20) ameuawa kwa kukatwa katwa na mapanga baada ya kufumaniwa akitaka kufanya mapenzi na na mke wa mtu.

Rombo. Mkazi wa kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Juvenal Claudi (20) ameuawa kwa kukatwa katwa na mapanga baada ya kufumaniwa akitaka kufanya mapenzi na na mke wa mtu.

Taarifa zinadai kuwa kijana huyo aliyeuawa alikuwa akichati na mke wa mtu ambapo baadaye mume wa mwanamke huyo, Riziki Shirima (22) alidaka simu ya mkewe na kukuta meseji za mapenzi.

Baada ya kukuta meseji hizo, mwanaume huyo aliweka mtego kwa kuendelea kumtumia meseji kijana huyo aliyeuawa, akijifanya yeye ndio mwanamke huku akimtaka kuja nyumbani jambo ambalo alifanya hivyo.

Baada ya kijana huyo kufika nyumbani alianza kushambuliwa kwa kukatwa mapanga na baadaye kufariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoani wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema tukio lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 4 na kusema baada ya mwanaume huyo kufanya mauaji alijisalimisha mwenyewe polisi.

"Ni kweli hili tukio limetokea katika kijiji cha Kibaoni wilaya ya Rombo ambapo mwanaume alimfumania mkewe nyumbani kwake akiwa na huyu kijana aliyeuawa wakitaka kufanya mapenzi," amesema Kamanda Maigwa

Kamanda Maigwa amesema jeshi la polisi linaendelea kumshikilia muuaji baada ya kujisalimisha mwenyewe polisi.