Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikopo ya mifugo NMB yavuka Sh180 bilioni

Muktasari:

  • NMB Bank imetoa zaidi ya Sh180 bilioni kufadhili sekta ya mifugo nchini, ikilenga kuongeza uzalishaji, ajira na masoko. Serikali imesisitiza kushirikiana na sekta binafsi kutatua changamoto ya malisho huku wafugaji wakihimizwa kutumia elimu na mikopo kuboresha biashara zao kwa tija zaidi.

Chalinze. Zaidi ya Sh180 bilioni zimetolewa na NMB Bank Plc kufadhili wafugaji na biashara katika mnyororo wa thamani wa mifugo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa kibiashara, ajira na upatikanaji wa masoko nchini.

Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Tri-Nations Livestock Expo 2026 katika viwanja vya Mbogo Ranches, Ubena Zomozi wilayani Chalinze, mkoani Pwani. NMB ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo kwa mwaka wa nne mfululizo.

Maonesho hayo, yanayowakutanisha wafugaji, wawekezaji, wanunuzi, taasisi za fedha na wadau kutoka Tanzania, Kenya na Namibia, yalifunguliwa na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba.

Mponzi amesema NMB imejenga mkakati wa kufadhili sekta ya mifugo kutoka ngazi ya mfugaji mmoja mmoja hadi biashara za kati na kubwa zinazojihusisha na uzalishaji wa malisho, unenepeshaji, uzalishaji wa mifugo bora, usindikaji na masoko.

“NMB ilikuwa benki ya kwanza nchini kuanzisha mikopo maalumu kwa wafugaji kwa riba nafuu ya asilimia tisa. Hadi Juni 2026, tumetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh180 bilioni kwa ajili ya unenepeshaji wa mifugo, uzalishaji wa malisho, ununuzi wa mbegu bora na ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya ufugaji,” alisema Mponzi.

Amesema kupitia mkakati wake wa agribusiness na agri-wholesale, benki hiyo inalenga kufadhili mnyororo mzima wa thamani, ikiwemo wafugaji, wazalishaji wa malisho, wanunuzi, wasindikaji na biashara kubwa zinazohudumia sekta ya mifugo.

Akifungua maonesho hayo, Waziri Mkuu Dk Nchemba amesema uhaba wa malisho unaendelea kuwa changamoto kubwa kwa wafugaji, hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kutafuta ufumbuzi wa kudumu.

“Suala la uhaba wa malisho ya mifugo ni dhahiri, na ndiyo maana Serikali imejizatiti kufanya kazi na wadau mbalimbali katika kutatua changamoto hii,” alisema Dk Nchemba.

Waziri Mkuu amewataka wafugaji kutumia elimu, teknolojia na uzoefu unaopatikana katika maonesho hayo kuboresha ufugaji, kuongeza tija na kuendesha shughuli zao kwa misingi ya kibiashara.

Mponzi amesema upatikanaji wa mikopo unapaswa kwenda sambamba na elimu ya fedha, usimamizi wa biashara, bima na ufahamu wa masoko ili wafugaji waweze kuwekeza, kurejesha mikopo kwa wakati na kupanua shughuli zao.

Katika maonesho hayo, NMB inatoa elimu ya fedha, ushauri wa biashara na taarifa kuhusu mikopo, bima ya mifugo na huduma za kidijitali kwa wafugaji na wadau wengine wa sekta hiyo.

Benki hiyo imesema itaendelea kutumia mtandao wake wa matawi 248, mawakala zaidi ya 75,000 na huduma za kidijitali kusogeza huduma za kifedha karibu zaidi na wafugaji, hususan waliopo maeneo ya vijijini na mbali na matawi ya benki.

Hatua hiyo inalenga kuunganisha wafugaji na mitaji, bima, maarifa na masoko ili sekta ya mifugo iongeze mchango wake katika kipato cha wananchi na ukuaji wa uchumi wa Taifa.