Audax: Tija ya Nanenane inatuhusu wadau wote
Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Jukwaa la Wadau wa Kilimo Lisilo la Kiserikali (Ansaf), Audax Lukonge.
Muktasari:
- Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Jukwaa la Wadau wa Kilimo Lisilo la Kiserikali (Ansaf), Audax Lukonge amesema tija ya maonyesho ya Nanenane inapimwa katika ushiriki wa wadau wa Sekta binafsi na umma katika kuchochea uzalishaji wenye tija, taarifa za mageuzi ya kiteknolojia na fursa za masoko.
Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji mstaafu wa Jukwaa la Wadau wa Kilimo Lisilo la Kiserikali (Ansaf), Audax Lukonge amesema tija ya maonyesho ya Nanenane inapimwa katika ushiriki wa wadau wa Sekta binafsi na umma katika kuchochea uzalishaji wenye tija, taarifa za mageuzi ya kiteknolojia na fursa za masoko.
Mbali na Lukonge, msemaji sekta ya uvuvi, Kilimi na Mifugo ACT Wazalendo Abdallah Mtutura ameshauri Serikali kufungamanisha sekta ya viwanda na kilimo kwa lengo la kuongeza tija ya uzalishajikupitia soko linalotokana na mahitaji ya viwanda vya ndani.
“Mfano korosho, asilimia 98 ys korosho yote inayozalishwa hapa nchini inaoelekqa nchini kwenda kubanguliwa,” amesema Mtutura aliyetoa mfano wa zao la korosho linalosafirishwa bila kuongezewa thamani hatua inayopunguza manufaa kwa mkulima na taifa kwa ujumla.
Mtutura ametoa kauli hiyo leo Agosti 9, 2023 wakati wa mjadala wa Mwananchi Twitter space iliyoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL), ukihusisha mada isemayo, ‘Je maonyesho ya Nanenane yanajitosheleza kuwa mwaarobaini wa changamoto za wakulima nchini?
“Kwa hiyo ufungamanishaji wa kilimo na viwanda ungeongeza tija kubwa sana na hata hawa wamachinga ambao sasa wanatoka vijijini kwenda mijini wangepungua kwa sababu wanaoondoka vijijini kwa sababu wanaona kilimo hakina tija,“ amesema Mtutura