Baba ambaka bintiye wa kambo

Baba ambaka bintiye wa kambo

Muktasari:

  • Baba wa kambo ambaka binti wa mkewe mwenye miaka saba kwa kumrubuni na maandazi na juisi ya Sh500

Geita. Jeshi la Polisi wilayani Geita linamshikilia Vicent Said (27) mkazi wa Kata ya Magenge kwa tuhuma za kumbaka mwanaye wa kambo mwenye umri wa miaka saba.

Tukio hilo limetokea Julai 2 katika Kijiji cha Sobora ambako mtuhumiwa anadaiwa kumrubuni mtoto huyo kwa maandazi na juisi ya Sh500.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Henry Mwaibambe amesema mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

Kamanda amesema baada ya tukio hilo wapo watu wanaotaka kuharibu ushahidi ili mtuhumiwa aachiwe huru na kuwatahadharisha kuacha juhudi hizo mara moja kwani polisi hawatozifumbia macho ili haki itendeke.

Akizungumza na gazeti hili mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho, alisema baba yake huyo amekuwa akimfanyia kitendo hicho mara kwa mara na pindi anapomfanyia humfunga mdomo na akimaliza humnunulia maandazi na juisi.