Baba atuhumiwa kuwabaka watoto wake, kesi yakwama

Jackson Ole Naiko (57) mkazi wa Kijiji cha Ndaleta Kata ya Njoro Wilayani Kiteto akiwa chini ya uangalizi wa Askari Polisi Kiteto akitoka mahakama ya wilaya hiyo baada ya kuahirishwa kesi yake ya ubakaji. Picha na Mohamed Hamad Kiteto.

Muktasari:

  • Katika kesi hiyo, Jackson Ole Naiko (57) anatuhumiwa kuwabaka kubaka watoto wake watano wa kuwazaa mwenyewe.

Kiteto. Mkazi wa Kijiji cha Ndaleta Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, Jackson Ole Naiko (57), leo Aprili 4 amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwabaka watoto wake wa kuwaza watano.

Hata hivyo, kesi hiyo imeshindwa kuendelea na kuahirishwa hadi April 13, 2023 kwa kilichoelezwa kuwa mwendesha mashtaka wa Serikali hakuwepo kwa kuwa amepata msiba.

Awali akizungumza mahakamani hapo, Hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Mossi Sasy, ameelezwa kuwa kesi hii ilikuwa iendelee kusikilizwa.

Amesema upande wa Jamhuri ulipaswa kuendelea kuwasilisha ushahidi wao na kilichobaki ni mashahidi muhimu wawili ambao nao walifika Mahakamani hapo kutoa ushahidi wa kesi hiyo.

Hata hivyo, amesema mwendesha mashitaka wa Serikali amepata msiba.

Mshtakiwa Jackson Ole Naiko aanatuhumiwa kuwabaka watano wake kwa nyakati tofauti kinyume na kifungu cha 158 (1) (a) cha sheria ya Makosa ya Jinai na sura ya 16 Kanuni ya adhabu.

Hakimu Sasy amewataka mashahidi hao kufika mahakamani hapo April 13, 2023 mahakamani kwa ajili ya kukamilisha ushahidi huo.