Baba kortini kwa kufanya mapenzi, kumpa ujauzito binti yake

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Hamis Said (37), mkazi wa Mtaa wa Nkokoto Wilaya ya Igunga amefikishwa mahakamani kwa kosa la kumpa ujauzito mtoto wake mwenye umri wa miaka 16.

Tabora. Hamis Said (37), mkazi wa Mtaa wa Nkokoto Wilaya ya Igunga amefikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya mapenzi na kumpa ujauzito mtoto wake mwenye umri wa miaka 16.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Edda Kahindi, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Albanus Ndunguru mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka mawili ambapo shtaka la kwanza ni kufanya mapenzi na harimu wake.

Katika shtaka la pili, mshtakiwa anadaiwa kumpa ujauzito mtoto wake (jina linahifadhiwa). Makosa yote ni kinyume cha Kifungu cha 158 (1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 mapitio ya 2022.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kwa siku tofauti kati ya mwaka 2018 hadi Juni, 2023.

Mwendesha mashtaka huyo ameiambia Mahakama kuwa ilipofika Juni, 2023 mshtakiwa alimpa ujauzito mtoto wake (jina linahifadhia) kinyume cha Kifungu cha 60 A (3) cha Sheria ya Elimu Sura ya 353 ya mwaka 2019.

Mshtakiwa amekana mashtaka dhidi yake na shauri hilo kuahirishwa hadi Oktoba 20, 2023 itakapotajwa kwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali baada ya upande wa mashtaka kuiambia Mahakama kuwa upelelezi umekamilika.

Mshtakiwa amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kusaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni.