Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baba Mtakatifu akubali ombi la Askofu Lebulu kujiuzulu

Muktasari:

Hivi karibuni Askofu Massawe  aliteuliwa kuwa msimamizi wa kitume Jimbo Katoliki la Mbulu.

Dar es Salaam. Baba Mtakatifu Francis amekubali ombi lililowasilishwa kwake na Askofu Mkuu Josephat Lebulu wa Jimbo Kuu la Arusha, Tanzania la kujiuzulu.

Pia, amemteua Askofu Isaac Massawe wa Jimbo Katoliki Moshi, kuwa Askofu Mkuu mpya wa Jimbo Kuu la Arusha.

Kwa mujibu wa redio Vatican, Askofu Mkuu mteule Massawe alizaliwa Juni 10, 1951 huko Mango, Jimbo Katoliki la Moshi.

Alipata upadri Juni 29,1975 na Novemba 21, 2007 aliteuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedict XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi na aliwekwa wakfu Februari 22,2008 na Kardinali Polycarp Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam akisaidiana na Askofu Mkuu Lebulu na Askofu Amedeus Msarikie (sasa marehemu) wa Jimbo Katoliki la Moshi.

Hivi karibuni, aliteuliwa kuwa msimamizi wa kitume Jimbo Katoliki la Mbulu.