Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balozi wa Marekani mgeni rasmi kongamano la wanawake nchini

New Content Item (1)

Kutoka kushoto ni mjumbe Mtendaji wa Taasisi ya Accelerate Business Group, Teddy Chamshama akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Bernice Fernandes na kulia ni muuguzi Mwandamizi na utawala kutoka kliniki ya Premier Care, Emma Kamande wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Picha na Hadija Jumanne

Dar es Salaam. Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la wanawake wajasiliamali na waliofanikiwa kiuongozi na kiuchumi kupitia nyanja mbalimbali za kazi wanazofanya.

Kongamano hilo la siku moja limeandaliwa na Taasisi ya Accelerate Business Group na litafanyika Machi 18, 2023 jiji hapa, huku likienda sambamba na maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani.

Pamoja na mambo mengine, kongamano hilo litakaloshirikisha wanawake zaidi ya 300, litajadili nafasi ya mwanamke katika uongozi, harakati za kimaendeleo, kuimarisha haki zao, changamoto wanazopitia katika kukuza uchumi na namna ya kukabiliana nazo.

Pia wanawake waliofanikiwa kushika nafasi za juu za uongozi, watatoa ushuhuda na siri za mafaniko yao hadi kupenya na kuwa katika nafasi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari,  Mkurugenzi wa Taasisi Accelerate Business Group, Bernice Fernandez alisema lengo la kongamano hilo ni kutoa fursa kwa watendaji, wajasiliamali kukutana kwa pamoja, kujadiliana na kujifunza kutoka kwa viongozi wazoefu alifanikiwa na wenye mawazo ya kipekee waliojitolea kuboresha hali za Wanawake katika jamii.

Fernandez alisema malengo mengine ni kujadili mikakati ya kuvunja vikwazo vinavyokwamisha maendeleo ya Wanawake pamoja na kutambua fursa za kusaidia mipango ya kuwawezesha wanawake.

"Kongamano hili linalokwemda kwa jina la Accelarate Executive Women's Breakfast litatoa fursa kwa washiriki kubadilishana mawazo, kutoa maoni yao juu ya uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzoefu wa kila mmoja" alisema Fernandez.

Baadhi ya wazungumzaji wakuu katika Kongamano hilo kutoka kampuni na mashirika mbalimbali kuwa ni Mwakilishi Mkazi wa wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake( UN WOMEN) Hodan Addou;  Meneja Uhusiano kutoka Kampuni ya Barrick Gold, Georgia Mutagahywa na Balozi mpya wa Marekani nchini Michael Battle ambaye siku hiyo atazungumza kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe .

Awali, Mjumbe Mtendaji wa Taasisi hiyo, Teddy Chamshama alisema wanawake wanapitia shida nyingi, ndio maana taassis yao imeandaa siku hiyo ili kuwapa nafasi wanawake kwa sababu ukimpa fursa mwanamke unakuwa umeinua uchumi.

"Tunarajia Kongamano hili litatoa ufahamu na msukumo mkubwa kwa washiriki wote katika kuchangia sababu za uwezeshaji wa wanawake katika jami yetu" alisema

Muuguzi Mwandamizi na utawala kutoka klinik ya Premier Care, Emma Kamande, alisema watakuwepo kwa ajili ya kutoa kuwafanya uchunguzi wa saratani ya matiti wanawake, kupima uzito na kutoa ushauri.

"Tumegundua wanawake wengi wanajisahau kupima afya zao kutokana na kuwa na majukumu ya ujenzi wa taifa" alisema Kamande.