Bandari ya uvuvi kuleta mabadiliko Kilwa

Muktasari:

  • Ujenzi wa bandari ya uvuvi ya kisasa wilayani Kilwa mkoani Lindi unatarajiwa kuleta mabadiliko chanya kwa wavuvi kufuatia fursa zitakazopatikana ikiwemo upatikanaji wa soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Pwani. Ujenzi wa bandari ya uvuvi ya kisasa wilayani Kilwa mkoani Lindi unatarajiwa kuleta mabadiliko chanya kwa wavuvi kufuatia fursa zitakazopatikana ikiwemo upatikanaji wa soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Thomas Safari alipokuwa akizungumza katika warsha ya utoaji elimu kwa wavuvi na wadau wa usafirishaji kwa njia ya maji iliyoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) leo Jumatano Septemba 28, 2022 wilayani humo.

Amesema bandari hiyo inategemewa kuwa kubwa kuliko zote kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati lakini pia itakua na tija kwa wananchi wa Kilwa na Mkoa wa Lindi kwa ujumla kwasababu shughuli za uvuvi zitaongezeka na hivyo upatikanaji wa samaki utakuwa mkubwa na kuchangia mzunguko wa fedha kuongezeka.

"Kwa kuwa wakazi wengi wa hapa shughuli zao kubwa ni uvuvi watakuwa wamepata sehemu ya kupeleka samaki wao ambao watawavua kwa utaratibu wa vyombo vya kisasa na watakuwa ni wasafi na bora kuliko wale wanaovuliwa kienyeji.

Akijibu kuhusu uamuzi wa Serikali kujenga bandari katiaka wilaya hiyo amesema

KIlwa kuna kina kirefu lakini pia kazi ya ujenzi itawa ni ya gharama nafuu kuliko ingejengwa Bagamoyo ambapo kina chake ni kifupi.

Safari ameongeza kuwa sababu nyingine iliyochagiza maamuzi hayo ya Serikali ni kuhakikisha shughuli za uvuvi zote zinahamia upande huo ili taasisi zote zinazofanya shughuli hizo zihamishiwe huko ili kuhakikisha upatikanaji wa samaki unakuwa unatumika kwa uhakika zaidi kwa ajili ya maendeleo.