Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bashe, Mpina uso kwa uso, wakubaliana kuacha siasa

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akilima kwa kutumia trekta akiwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (kushoto) walipokutana leo Septemba 13, 2024 katika jimbo la Kisesa.

Muktasari:

  • Waziri wa Kilimo Hussein Bashe na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina wamekubaliana kuweka tofauti zao pembeni na kushirikiana kwa maendeleo ya nchi.



Dar es Salaam. Baada ya kutoleana vijembe ndani na nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatimaye Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina wamekutana uso kwa uso.

Bashe yupo kwenye ziara ya kikazi kwenye maeneo mbalimbali nchini na leo Ijumaa, Septemba 13, 2024 amefika katika Jimbo la Kisesa linaloongozwa na Mpina na kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wakulima na maofisa ugani.

Akiwa jimboni humo, Bashe amemtaka Mpina kuacha siasa kwenye zao la pamba kwa kuwa Serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, inahitaji kuona fedha zinazotengwa zinanufaisha wakulima wa zao hilo.

“Rais Samia amefanya kazi kubwa katika kilimo, Mpina amesema hapa na mimi nataka nisisitize tuweke mambo mengine pembeni, aache siasa na sitaki siasa katika zao la pamba.

Nafahamu zipo changamoto lakini tulipotoka sio tulipo, sitakubali mtu arudishe nyuma jitihada hizi wanaoteseka wananchi,” amesema Bashe na kuongeza: “Na mimi leo nimesimikwa kuwa mtemi wa Kisesa, hivyo Mpina akinitambia pale bungeni kwa kuingia na fimbo ya uchifu nami nitaingia na yangu.”

Katika ziara yake jimboni humo, Bashe amekabidhi trekta 40 huku akiwataka maofisa kilimo na ugani kuacha kukaa mjini na kuishi vijijini ili kuwasaidia wakulima na kufikia malengo ya Serikali ya kukifanya kilimo chenye tija.

Pia, ameahidi kuwa Serikali itarejesha kitalu cha mbegu kuwapatia ruzuku ya dawa za wadudu katika zao la mahindi na pembejeo za pamba.

Kwa upande wake, Mpina amesema yuko tayari kuweka pembeni tofauti zake na Bashe na kuungana kwenye masuala ya maendeleo.

Amesema anatambua kuwa wana tofauti na Bashe, hali iliyowafikisha hadi mahakamani, lakini yupo tayari kushirikiana naye katika masuala ya maendeleo.

Naye upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kennan Kihongosi amemuhakikishia Bashe kuwa yeye ndio mwenye dhamana na mkoa huo, hivyo hawezi kuvumilia watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kwa kuingiza masuala ya maendeleo.

“Nimetumwa kazi na Rais Samia, Simiyu ni ya kwanza ama ya pili katika kuzalisha pamba, hivyo kwa wananchi ni zao la kiuchumi, nisingependa wanasiasa watumie zao hilo kutafuta umaarufu. Shida zinazosemwa katika zao hilo si za kweli wananchi wa Kisesa msikubali kutumika,” amesema Kihongosi.

Kwa muda mrefu, Bashe na Mpina wamekuwa wakivutana ndani na nje ya Bunge wakionekana kutofautiana kwenye masuala mbalimbali.

Kwa sasa Mpina anatumikia adhabu ya kukosa vikao vya Bunge baada ya kusimamishwa kwa kutoa kauli alizozitoa dhidi ya Bashe kuhusu taarifa za uingizaji wa sukari kutoka nje na ile inayozalishwa kwenye viwanda vya ndani.