Bendera za ACT zamwagwa Pemba

Muktasari:

  • Saa chache baada ya Maalim Seif Sharif Hamad kuwasili katika ofisi za ACT-Wazalendo zilizopo Vuga, Unguja, bendera za chama hicho zimewasili kisiwani Pemba

Pemba. Saa chache baada ya Maalim Seif Sharif Hamad kuwasili katika ofisi za ACT-Wazalendo zilizopo Vuga, Unguja, bendera za chama hicho zimewasilini kisiwani Pemba.

Leo Alhamisi Machi 21, 2019 Mwananchi limeshuhudia ugawaji wa bendera katika ofisi mbalimbali za CUF ambazo sasa zinatumiwa na ACT baada ya aliyekuwa katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi mbalimbali kukihama chama hicho.

Hadija Anuar,  kaimu mwenyekiti Ngome ya ACT- Wazalendo Pemba amesema wamelazimika kufanya haraka kutokana na uhitaji wa bendera katika matawi mbalimbali.

Kuhusu mapokezi ya Maalim Seif na kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe wanaotarajiwa kuanza ziara ya siku nne kesho kisiwani Pemba,  Hadija amesema maandalizi yamekamilika na kuwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kuwapokea.