Benki ya Efatha yafungwa baada ya taarifa ya BoT
Muktasari:
BoT imezifungia benki tano keanzia leo ikiwemo ya Efatha
Dar es Salaam. Benki ya Efatha imefungwa na hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia ndani.
Nje ya benki hiyo zimebandikwa barua za Benki Kuu ya Tanzania(BoT) ambazo zinafafanua hatua iliyochukua na kutoa maelekezo kwa watu wenye amana katika benki hiyo.
Kila mteja anayefika anaelekezwa kwenye tangazo lililobandikwa ili kusoma na kupata maelezo zaidi.
Hakuna watu waliofika kupata huduma na benki hiyo inalindwa na kampuni moja ya ulinzi pamoja na askari polisi.