Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bibi afariki dunia akiruka ghorofani

Muktasari:

  • Mkazi wa Unguja, Zanzibar, Rehema Chande (70) amefariki dunia baada ya kuruka kutoka ghorofa ya pili nyumba anayoishi wakati akijiokoa dhidi ya moto uliowaka ndani ya nyumba hiyo.


Unguja. Mkazi wa Unguja, Zanzibar, Rehema Chande (70) amefariki dunia baada ya kuruka kutoka ghorofa ya pili nyumba anayoishi wakati akijiokoa dhidi ya moto uliowaka ndani ya nyumba hiyo.

Tukio hilo limetokea leo Jumanne, Agosti 29, 2022 saa 3.30 asubuhi katika Shehia ya Kiponda Wadi ya Malindi, Mji Mkongwe ambapo bibi huyo aliruka na mjukuu wake Nabili Issa Ramadhani (5) ambaye amejeruhiwa na kulazwa Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar, Rashid Mzee Abdallah amethibitisha tukio hilo na kwamba walipofika eneo la tukio walimkuta bibi huyo na mjukuu wake lakini walipofikishwa hospitalini daktari alisema tayari Rehema ameshafariki dunia.

"Rehema aliruka kujiokoa na moto baada ya kutanda na kushindwa kutoka ndani, kwa hiyo aliporuka yeye kapoteza maisha lakini mjukuu wake amejeruhiwa na anaendelea na matibabu," emesema  Abdallah.

Kuhusu athari zingine, Mkuu huyo wa Kikosi cha Zimamoto, amesema bado wanaendelea na kazi ya kuuzima moto huo kutokana mazingira ya eneo hilo kutokuwa rafiki.

Sheha wa Shehia hiyo, Juma Khamis Makame amesema bibi huyo alikuwa anaishi na mjukuu wake na watoto wengine lakini kwa wakati huo hawakuwa ndani.