Bodi ya Mfuko wa Barabara yazuia pesa kwenda Kinondoni

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Joseph Haule.

Muktasari:

Barabara hiyo ya urefu wa kilometa 2 ilitakiwa kukamilika kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Machi-Juni 2015 ila mpaka mwaka 2016 ilikamalika kwa urefu wa mita 700 tu.

Dar es Salaam. Bodi ya Mfuko wa Barabara imesimamisha kupeleka fedha za mfuko huo katika Manispaa ya Kinondoni baada ya kubaini ujenzi wa barabara chini ya kiwango eneo la Masjid-Quba uliogharimu Sh 3.3 bilioni.

Barabara hiyo ya urefu wa kilometa 2 ilitakiwa kukamilika kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Machi-Juni 2015 ila mpaka mwaka 2016 ilikamalika kwa urefu wa mita 700 tu.

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Joseph Haule amesema fedha hizo zipo Halmashauri ya Kinondoni na tayari mkandarasi amelipwa Sh 200 milioni.

"Halmashauri hii imekuwa na mapungufu ya miradi mingi ya barabara mfano Barabara za Mabatini-police, Akachube, Sayansi zote zimeharibika mapema," alisema Haule.