Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bomoabomoa yaacha simanzi Mabwepande

Muktasari:

Ni hali ya taharuki kwa baadhi ya wakazi wa Mabwepande Wilaya na Kinondoni wanaodaiwa kujenga eneo lisiloruhusiwa, baada ya nyumba zao kubomolewa huku wakiwa hawajui la kufanya na familia zao.





Dar es Salaam. Ni hali ya taharuki kwa baadhi ya wakazi wa Mabwepande Wilaya na Kinondoni wanaodaiwa kujenga eneo lisiloruhusiwa, baada ya nyumba zao kubomolewa huku wakiwa hawajui la kufanya na familia zao.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi kuhusu ubomoaji huo ulioanza Julai 4, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Hanifa Hamza alisema ubomoaji unafanyika kwa wale waliovamia maeneo ya Serikali huku akieleza notisi ya kufanya hivyo waliitoa tangu Aprili mwaka huu.

“Tulifika Mabwepande kama Serikali ya Wilaya tukazungumza na wananchi, nao walieleza malalamiko yao na tuliwataka wote waliovamia maeneo wahame kwa sababu yanatakiwa kuendelezwa,” alisema.

Kuhusu baadhi ya nyumba kutokuvunjwa, Mkurugenzi huyo alisema hafahamu hilo isipokuwa anatambua wale wote waliovamia nyumba zao zinapaswa kuvunjwa. “Kama kuna watu hawavunjiwi suala hilo nitawasilisha kwenye kikao chetu cha kamati ya ulinzi na usalama, manispaa tunasimamia sheria wote lazima waondoke,” alisema.


Wananchi waeleza

Mwananchi limefika eneo hilo na kushuhudia wananchi wakiwa wamekaa vikundi na familia zao huku nyuso zao zikiwa na huzuni huku baadhi wakilia wakidai wametumia gharama kubwa kujenga nyumba hizo ikiwemo kuchukua mikopo benki.

“Ndoto ya kumiliki nyumba kuishi na familia yangu ilishatimia. Nimetumia Sh30 milioni hadi kukamilisha, cha ajabu zimekuja kuvunjwa bila taarifa, tena kwa kupigwa mabomu. Nimebaki kama nilivyo na watoto wangu wanane,” alisema Saimon Nkya.

Alisema walianza kuishi eneo hilo mwaka 2003 na Serikali ya wilaya iliwapimia maeneo hayo na kuwapelekea huduma muhimu kama maji na umeme.

Alfonsia Kisanga, mama wa watoto watano alisema amelazimika kuwasafirisha watoto wake kwenda mkoani kuishi kwa ndugu ingawa bado wanasoma.

“Watoto wangu wanasoma chuo sitaki waendelee kupata shida hapa, sina makazi tena na mpango wa kuwasomesha nimesitisha kwa muda hadi nipate makazi ya kudumu . Serikali haitutendei haki hata kidogo.

“Tunaiomba Serikali ichukue hatua, kwani tunahangaika na familia zetu na hatuna sehemu ya kujihifadhi. Matajiri nyumba zao zimeachwa, ila sisi wa hali ya chini ndiyo zimebomolewa,”alisema.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Kinondo ambaye hakutaka kutajwa jina alisema kwenye mtaa wake nyumba 400 zimebomolewa na siku wanakwenda hawakutoa taarifa, jambo lililosababisha kuleta taharuki kwa wananchi.