Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bosi NIC atenguliwa, Rais Magufuli amteua mpya

Rais wa Tanzania, John Magufuli

Muktasari:

  • Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu na Ikulu ya Tanzania imesema Rais wa nchi hiyo, John Magufuli amemteua Elirehema Doriye kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuchukua nafasi ya Sam Kamanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amefanya uteuzi wa Dk Elirehema Doriye kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Taarifa iliyotolewa jana usiku Jumatatu Julai 29, 2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania imesema Dk Doriye anachukua nafasi ya Sam Kamanga ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Taarifa hiyo imesema kabla ya uteuzi huo, Dk Doriye alikuwa Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) nchini Tanzania na uteuzi wake umeanza jana Jumatatu.