Bosi wa Vodacom Tanzania afikishwa mahakamani

Muktasari:

Leo Jumatano, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Hisham Abdel Hendi na wenzake wanane wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa  Kampuni ya Vodacom Tanzania, Hisham Abdel Hendi na wenzake wanane wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka kumi yakiwamo ya kuongoza mtandao wa kihalifu na kuisababishia Serikali hasara ya Sh5.8 bilioni.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakama hapa leo Jumatano Aprili 3, 2019 na kusomewa mashtaka hayo katika kesi ya uhujumu uchumi namba 20/2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Endelea  kufuatilia Mwananchi kujua kinachojiri mahakamani hapo