Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

BOT yamaliza sakata la Yetu Microfinance, sasa chini ya NMB

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania imehamisha mali na madeni ya Yetu Microfinance Bank PIc kwenda NMB Bank Plc baada ya kuiweka chini ya usimamizi wake kwa miezi mitano.

Hii ina maana kwamba wenye amana na wadai wengine wa Yetu Microfinance Bank Pic watapewa taarifa ya namna na siku watakayoanza kupata huduma za kibenki kupitia benki ya NMB.

Itakumbukwa kuwa Disemba 12, 2022 BOT iliweka chini ya usimamizi wake Yetu Microfinance Bank Pic kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili ya mtaji na ukwasi.

Taarifa iliyotolewa leo na Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba inaeleza kuwa kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 594 cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, mchakato wa kupata suluhisho la Yetu Microfinance Bank Pic umekamilika, na uhamishaji wa mali na madeni kwenda benki nyingine ndio hatua stahiki iliyofikiwa.

Taarifa hiyo imewasisitiza wateja wote wenye mikopo kuwa wanatakiwa kuendelea kulipa marejesho yao kwa mujibu ya mikataba ya mikopo hiyo.

Kwa mujibu wa gavana Tutuba taasisi hiyo ya Serikali itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya kibenki.