BREAKING NEWS: Wanafunzi wanane wafa ajalini Mtwara, Rais Samia awalilia

Basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Msingi ya King David baada ya kutumbukia shimoni na kusababisha vifo vya watu 10 wakiwamo wanafunzi wanane. Picha na mtandao

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kufuatia vifo vya watu 10 wakiwamo wanafunzi wanane vilivyosababishwa na ajali ya basi la shule.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kufuatia vifo vya watu 10 wakiwamo wanafunzi wanane vilivyosababishwa na ajali ya basi la shule.

Ajali hiyo imetokea leo Jumanne Julai 26, 2022, baada ya basi lililokuwa limebeba wanafunzi wa Shule ya Msingi ya King David kutumbukia shimoni.

Katika Salamu zake za pole alizoziandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia amesema; “Nimesikitishwa na vifo vya wanafunzi 8 wa shule ya msingi ya King David na watu wazima 2 vilivyotokea leo asubuhi huko Mtwara Mikindani baada ya gari la shule kutumbulikia shimoni. Nawapa pole wafiwa, Mkuu wa Mkoa na jamaa. Mwenyezi Mungu awarehemu marehemu na kuwaponya majeruhi”.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Hamad Nyembea amesema kuwa wamepokea majeruhi 18 na vifo vya watu 10.

Katika vifo hivyo watoto wa kike ni 5 wakiume ni 3 na watu wazima ni wawili.

PIA SOMA: Polisi yathibitisha wanafunzi 31 kufariki katika ajali Arusha


Habari zaidi kukujia