Kamanda wa Polisi asema chanzo cha ajali iliyoua 35 ni mwendo kasi

Arusha. Kamanda wa Polisi, mkoa wa Arusha amesema uchunguzi wa awali wa ajali iliyoua zaidi ya watu 35 wakiwamo wanafunzi 32,  wilayani Karatu umeonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi.

Kamanda Mkumbo amesema hadi sasa wanafunzi watatu waliojeruhiwa katika ajali hiyo wamefikishwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.

 Alisema majeruhi wengine wamefariki njiani wakati wakikimbizwa hospitali.