Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM yaonya wanaohujumu shule za Wazazi

Muktasari:

  • Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mbeya, Hakimu Mwalupimbi wakati akimkaribisha Mbunge wa Lupa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, Masache Kasaka kwenye mahafali ya 33 ya shule ya sekondari Mbalizi.

Mbeya. CCM wilayani Mbeya imeonya baadhi ya wanachama wa chama hicho wanaoyumbisha uendeshaji wa shule za sekondari zinazomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi na kuwataka wajumbe wa bodi kuanza kuwashughulikia.

Mwalupimbi amesema Oktoba 13, 2023 mara baada ya kushiriki mahafali ya 33 katika shule ya sekondari Mbalizi, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Lupa Masache Kasaka.

Amesema kuna watu wamekuwa vinara wa kuyumbisha maendeleo na kutaka wajumbe wa bodi kuanza kuwachukulia hatua kwani wanawakatisha tamaa wakuu wa shule hizo.

“Wapo wanasiasa wanakuja wanahamishwa shule hizi wanaziacha, sasa umefika wakati wale wachache wanaokuwa chanzo cha kuyumbisha wawajibishwe,” amesema

Hata hivyo, amempongeza Mkuu wa shule ya sekondari Mbalizi, Marco Shija kwa mchango wake wa kuboresha taaluma.

Amesema  uendeshaji mzuri wa taaluma umechochea ongezeko la wanafunzi kutoka 300 mpaka 800 kwa mwaka 2022/23 sambamba na kuongoza kimkoa kwa kipindi cha miaka miwili

Kwa upande wake Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka amesema uongozi mzuri ni pamoja na ubunifu wa kuwepo kwa mitaala mipya ya lugha za Kichina na Kifaransa.

“Uongozi wa shule umefanya kazi kubwa ya kuboresha taaluma kwani kwa matokeo ya mwaka jana ilishika nafasi ya kwanza kimkoa, licha ya kuwepo kwa changamoto za ufinyu wa maabara, uchakavu miundombinu ya zahanati na mahitaji ya kisima cha maji, amehaidi kushughulikia mapema kwa kuishirikisha Serikali,” amesema.

Katika hatua nyingine amesema kuhusu suala la maabara ataibana Serikali akichangia Sh1 milioni kwa ajili ya kuboresha baadhi ya changamoto.

Naye Mkuu wa Shule hiyo, Marco Shija amesema wanahitaji zaidi ya Sh48 milioni kwa ajili ya upanuzi wa maabara itakayochukua wanafunzi 120 wa masomo ya Sayansi.

“Maabara tuliyo ni ndogo inachukua wanafunzi 20 ambayo haikidhi mahitaji kulingana na idadi ya wanafunzi na kuomba Serikali kuliona hilo ili kuongeza kiwango cha taalum,” amesema.


Kuhusu hali ya taaluma

Shija amesema  kwa kipindi cha miaka miwili 2022/23 ufaulu kwa kidato cha pili ulikuwa asilimia 100 sambamba na kidato cha nne na mafanikio hayo ni kutokana na mifumo ya uandaaji wa mitaala ya kitaaluma.

“Kipindi cha mwaka 2022 Shule ilikuwa na wanafunzi 300 ambapo mwaka 2023 imeongezeka na kufikia 800 kati ya hao 384 wanaishi bweni na waliobaki ni kutwa.

Muhitimu kidato cha nne, Irene Chaula ameomba Serikali kupitia kwa Mbunge huyo kuchangia ujenzi wa chumba cha darasa la kujifunzia lugha za Kichina na Kifaransa ambayo imeanza kutolewa shuleni hapo.

Mmoja wa wazazi Rebecca Saimon, amesema   awali Shule za Jumuiya ya wazazi zilipoteza mwelekeo ambapo kwa kipindi cha miaka miwili zimekuwa zikifanya jambo ambalo limetusukuma kuleta watoto kupata elimu bora.