Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CDA yakanusha uvumi kuhusu uuzwaji wa viwanja Mkonze

Muktasari:

Tamko hilo limetolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Kaimu Meneja Uhusiano wa CDA, Angela Msimbira kutokana na kusambaa kwa ujumbe huo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) imekanusha  uvumi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uuzaji wa viwanja katika eneo la Mkonze lililopo mkoani Dodoma.

Tamko hilo limetolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Kaimu Meneja Uhusiano wa CDA, Angela Msimbira kutokana na kusambaa kwa ujumbe huo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Angela amesema taarifa hizo ambazo hazieleweki zimekuwa zikidai kuwa viwanja hivyo ni halali na ukinunua unapewa hati na CDA ambayo ndiyo imepewa dhamana ya ugawaji wa viwanja mkoani humo.

“Mamlaka yetu inapenda kuutarifu umma kuwa taarifa hizo si za kweli hivyo wananchi wanatakiwa kuzipuuza na kuendelea kufata utaratibu  kwani mamlaka hiyo ina utaratibu uliopangwa wa namna ya kupata viwanja vilivyo halali,”amesema  Angela.