Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chalamila: Wafanyabiashara Karikakoo hamkupaswa kwenda CCM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza na wafanyabiashara katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

Muktasari:

  • Wafanyabiashara hao waliandamana jana Alhamisi kwenda Ofisi za CCM Lumumba wakipinga kukatwa kwa majina ya watakaorejea soko la Kariakoo.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema kitendo cha wafanyabiashara wa soko la Kariakoo kuandamana kwenda ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) ni kujipofusha.

Hayo ameyasema leo Ijumaa Julai 12, 2024 alipokutana na wafanyabiara hao kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam.

Wafanyabiashara hao zaidi ya 800 jana Alhamisi  Julai 11, 2024, waliandamana kutoka Uwanja wa Mnazi Mmoja kwenda ofisi za CCM Lumumba, kupinga kuondolewa kwa wafanyabiashara waliokuwa sokoni hapo kabla halijaungua Julai 2021.

Walichukua uamuzi huo baada ya kupinga utaratibu Shirika la Masoko Kariakoo kutenga siku tatu kuanzia jana kuhakiki majina yao ambao hawapo kati ya yale yaliyotangazwa.

Mara baada ya kufika ofisi hizo za CCM kufikisha ujumbe hao, viongozi wa chama hicho tawala waliwaeleza watulie baada ya kuwa wanaimba nyimbo mbalimbali na kufunga barabara.

Wafanyabiahara wa Soko la Kariakoo wakiwa nje ya ofisi za CCM Lumumba jana Julai 11, 2024 jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwa hapo kwa takriban saa mbili, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo aliwaeleza RC Chalamila atawasililiza leo ofisini kwake.

Asubuhi ya leo Ijumaa, wafanyabiashara wamejitokeza kwa wingi katika ukumbi wa mkuu huyo wa mkoa kufikisha ujumbe wao na kumsikiliza atakachokieleza.

Chalamila amesema wafanyabiashara hao hawakupaswa kwenda CCM kwa kuwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa ipo na ndio inasimamia soko hilo.

"Mlichofanya  wafanyabiashara jana kwenda CCM ni sawa na mgonjwa wa malaria kwenda kwa mtu asiyetibu malaria.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ipo, mlipaswa kuja  hapa kwa kuwa ndio tunaolisimamia na siyo huko mlikokwenda," amesema Chalamila.

Akieleza hali ilivyokuwa hadi kuja na orodha ya majina ya watu 819 kati ya 1,891, amesema baada ya kufanya uhakiki wa awamu ya kwanza hao ndio waligundulika hawana mawaa.

Hata hivyo, amesema orodha nyingine iliyobaki bado inafanyiwa kazi na siyo kwamba wameachwa kabisa.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa   amesema kabla ya soko kuungua, kulikuwa na uholela usiokuwa na tija kwa mtu mmoja kuchukua vibanda zaidi ya kumi kuvipangisha na kujikuta soko hilo limemezwa na madalali.

"Kati yenu hapa wapo wafanyabiashara, wapo madalali jambo hili tutaelewa tu japo papo patakapouma na kwa utaratibu wa sasa wa soko niwaambie tumekata mzizi wa udalali," amesema Chalamila.


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari na matukio zaidi