Chanzo cha tatizo la tumbo kujaa gesi

Saturday May 14 2022
gesi pc
By Mwandishi Wetu

Kuwa na gesi tumboni au tumbo kujaa gesi si tatizo geni kwa wagonjwa wa kisukari, hasa wanaotumia dawa za vidonge kudhibiti kiwango cha sukari.

Lakini pia aina ya vyakula ni sababu nyingine ya kupata tatizo la tumbo kujaa gesi pamoja na tatizo la msongo wa mawazo. Magonjwa kama ulcerative colitis, celiac disease na IBS-inflammatory bowel syndrome huweza kusababisha kujaa gesi tumboni.

Dalili za tumbo kujaa gesi ni kama kupata homa, muwasho kwenye koo, maumivu sehemu za tezi hasa mwili kukosa nguvu na uchovu.

Kupata athari ya chakula fulani kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi. Maziwa, mayai na ngano vinaweza kuwa ni sababu ya tumbo kujaa gesi. Kama mwili unakataa aina fulani ya vyakula na unapata mcharuko kama kuvimba, kuharisha, ama kutapika basi usitumie chakula hicho. Kama mwili unapambana na maambukizi aidha ya bakteria, virusi, fangasi au vimelea wengine basi utapata tatizo la kujaa gesi tumboni kutokana na mpambano wa ugonjwa na seli nyeupe za damu.

Kupata gesi tumboni kutokana na vidonda ama uvimbe kwenye baadhi ya sehemu za mfumo wa chakula kama utumbo mdogo na utumbo mpana. Uvimbe unaweza kuzuia utolewaji wa uchafu na kuletekeza gesi na maji kukwama.

Moja ya dalili za saratani ya utumbo mpana na saratani ya mfuko wa mimba ni tumbo kujaa gesi. Ndio maana ni muhimu kuzungumza na daktari wako pale ambapo umejaribu kila njia ya kuondoa tatizo lako lakini bado halijaisha.

Advertisement

Ugonjwa wa kisukari unaweza kusababisha tumbo kujaa gesi, hasa kipindi cha hedhi, hivyo kabla ya kuanza kutumia dawa ni muhimu kuonana na daktari.

Ili kuepuka changamoto hiyo unatakiwa kuwa mwangalifu kwenye chakula na kuepuka vyakula ambavyo vitasababisha gesi, lakini pia kunywa maji ya kutosha na kupunguza au kukwepa msongo wa mawazo.


Mwandishi wa makala hii, Lucy Johnbosco ni mshauri wa wagonjwa wa kisukari.

Advertisement