China yaipa Tanzania Sh 97 bilioni

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage
Muktasari:
Akizungumza, Mwijage amesema waziri huyo amekuja na Ujumbe wa wafanyabiashara ili kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Viwanda vya chuma na vigae walivyowekeza nchini.
Dar es Salaam. Serikali ya China imeipatia Tanzania msaada wa Sh97 bilioni ili zisaidie kuboresha sekta za elimu na afya.Msaada huo umesainiwa leo kati ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage na Naibu waziri wa Biashara wa China,Qian Keming.
Akizungumza, Mwijage amesema waziri huyo amekuja na Ujumbe wa wafanyabiashara ili kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Viwanda vya chuma na vigae walivyowekeza nchini.
Waziri Mwijage amesema wameamua kuleta na msaada huo wa fedha ili kudumisha urafiki wetu kati ya Tanzania na China.