Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chongolo kufunga na mawaziri watano

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo.

Katavi. Ziara ya siku tano ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo mkoani Katavi inahitimishwa leo, huku mawaziri watano wakitarajiwa kupanda jukwaani kujibu changamoto zilizoibuliwa.

Mawaziri watatoa majibu au ufafanuzi wa kero hizo katika mkutano wa hadhara utakaofanyika Mpanda Mjini. Changamoto hizo ziliibuliwa kuanzia Oktoba 2, mwaka huu hadi jana katika wilaya tatu za mkoa huo za Mlele, Tanganyika na Mpanda.

Mawaziri hao ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko aliyeahidi kuwakilishwa na naibu wake, Judith Kapinga atakayezungumzia masuala yote ya umeme.

Wengine ni, Innocent Bashungwa (Ujenzi), Mohammed Mchengerwa (Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa-Tamisemi), Jerry Silaa (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na Jumaa Aweso (Maji).

Lengo la ziara hiyo ilikuwa kuimarisha uhai wa chama kwa kushiriki vikao ngazi ya shina, kukagua miradi ya maendeleo kama ya afya, elimu, kilimo, barabara na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya chama hicho ya mwaka 2020/2025.

Mara baada ya kutua Oktoba 2 mwaka huu na kuzungumza na viongozi wa chama hicho na Serikali, Chongolo alisema, "tunataka mtupatie changamoto na si kusifia tu, mkituonyesha changamoto, tutazichukua na kuzifanyia kazi ili uchaguzi ujao uwe mzuri."


Barabara, umeme

Kilichoibuliwa na wananchi, viongozi wa Serikali na wa CCM ni kusuasua kwa ujenzi wa barabara, mathalani ya Kibaoni-Mlele kilomita 50, Wilaya ya Mlele kwa gharama ya Sh88.7 bilioni inayojengwa na mkandarasi M/s China Railway Seventh Group Co. Ltd (CRSG) ikiwa nyuma ya utekelezaji kwa zaidi ya asilimia 30.

Mradi wa barabara ya kilomita 400 ya Ugalla, Kaliuwa (Tabora), Kahama (Shinyanga) na kukagua maandalizi ya ujenzi wa daraja linalotenganisha mkoa wa Katavi na Tabora nao kuliibuka malalamiko ya fidia kwa wananchi waliopisha ujenzi huo.

Kero ya maji kwa maeneo mbalimbali na makandarasi wanaotekeleza miradi kutokulipwa fedha, lakini pia Mradi wa Maji Katambike, Kata ya Ugalla kusuasua kwa kuwa asilimia 15, huku mkataba ukionyesha unapaswa kumalizika mwezi huu ni eneo ambalo Chongolo hakuliafiki.

Migogoro ya ardhi ya mipaka ya hifadhi na makazi ya wananchi kuwekwa alama hadi kwenye mashamba ya wananchi wa Wilaya ya Mlele na maeneo mengine mkoani humo ni eneo ambalo Waziri Silaa na wasaidizi wake watajibu.

Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Katavi, Iddi Kimanta alimwomba Chongolo kuweka msukumo wa kupatikana fedha za ujenzi wa bweni kwa kuwa wanafunzi wanatembea kilomita 30 kufuata shule.