Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Daktari bingwa ashindwa kufanya upasuaji Mtwara

Mganga Mfawidhi wa Ligula, Kariamel Wandi.

Muktasari:

  • Ukosefu wa vifaa vya upasuaji hospitalini umemkwamisha daktari huyo kufanya upasuaji

Daktari bingwa wa masikio, koo na pua, Jonas Ndasika ameshindwa kufanya upasuaji kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara.

Akizungumza baada ya kumaliza utoaji wa huduma za madaktari bingwa ulioandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mganga Mfawidhi wa Ligula, Kariamel Wandi amesema utoaji wa huduma hizo umeonekana wa kusua sua kutokana na baadhi ya vifaa kukosekana na katika hospital hiyo.

“Daktari bingwa wa masikio, koo na pua ndiyo daktari pekee ambaye ameshindwa kufanya upasuaji kwa sababu hospitali yetu ya Ligula haina vifaa hivyo,” amesema.

“Vifaa vya masikio, koo na pua hakuna kabisa katika hospitali yetu na huduma hii haijawahi kutolewa  kama iliwahi kutolewa labda miaka ya nyuma.”

Mganga huyo ameomba Serikali kuhakikisha hospitali ambazo zipo pembezoni zinakuwa na vifaa pamoja na madaktari ili kuweza kufanya kazi wa ufanisi mzuri zaidi.