Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dar mwenyeji mkutano wa uvuvi mdogo Afrika

Muktasari:

  • Serikali kwa ushirikiano na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la Chakula Duniani (FA0) wameandaa mkutano wa kimataifa wa sekta ya uvuvi na wavuvi wadogo ili kujadili changamoto zitakazopatiwa ufumbuzi ili sekta hiyo isonge mbele zaidi.

Dar es Salaam. Wadau wa sekta ya uvuvi Afrika watakutana jijijin hapa Juni 5 mpaka 7, 2024 kujadili namna ya kuwasaidia vijana na wanawake kufanya kazi hiyo kwa weledi.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 23, 2024 na Waziri  wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika jijini Dar es Salaam kuhusu mkutano ambao Tanzania ni mwenyeji,

Amesema mbali ya wadau, Rais  Samia Suluhu na mawaziri waandamizi wa sekta ya uvuvi barani Afrika watakuwa miongoni mwa watakaoshiriki mkutano huo.

Waziri Ulega amesema mkutano huo ulioandaliwa na Serikali kwa ushirikiano na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la Chakula Duniani (FAO) utajadili uvuvi mdogo na wavuvi wadogo wanaochukua asilimia 95 ya uvuvi hapa nchini katika bahari na maziwa.

Amesema mkutano huo utajadili pia hatima ya shughuli hiyo, kubadilishana uzoefu na maarifa, kipi kimepitwa na wakati kuboreshwa ili kuleta uendelevu wa rasilimali hiyo.

"Pia mkutano huo utaangalia maadhimisho ya miaka 10 ya mwongozo wa uvuvi mdogo na muundo wa kisera wa kusimamia uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji (ufugaji wa samaki), barani Afrika.

"Lakini pia tutaangazia juu ya fursa zilizopo za uchumi wa buluu hasa katika sekta za uvuvi na ufugaji samaki," amesema Waziri Ulega.

Kwa mujibu wa Ulega, mkutano huo unafanyika Tanzania kwa mara ya kwanza kwa bara la Afrika kwa kukutanisha nchi mbalimbali zikiwemo kutoka Kusini na Mashariki wa bara hilo  zitakazojadili uvuvi mdogo na hatma yake.

"Haya hayajatokea kwa bahati mbaya na Waswahili wanasema usione vyaelea, vimeundwa, mkutano unafanyika kutokana na jitihada za kidiplomasia ya uchumi inayotekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Mkutano huu utakuwa chachu kubadilisha uzoefu, fikra za kisasa za uvuvi za kufanya sekta hiyo kusonga mbele zaidi na endelevu sambamba na kukabiliana na uvuvi haramu," amesema.

Mbali na hilo, Waziri Ulega amesema kutakuwa na mjadala wa kusaidia makundi ya vijana na wanawake katika shughuli za uvuvi ili kujiingizia kipato ili kujenga kesho iliyo bora zaidi.

Amesema mchango wa sekta hiyo ni takribani asilimia 1.9 ya pato la Taifa na kutoa ajira za moja kwa moja takribani watu 230,000.

"Biashara ya samaki kwa mwaka inafika hadi Sh3.4 trilioni ambayo ni thamani ya mazao ya samaki. Samaki na viumbe wengine wa majini wana mchango mkubwa katika upatikanaji wa fedha za kigeni," amesema.

Waziri Ulega amesema mkutano huo utavutia uwekezaji, teknolojia za kisasa na kuwafanya wavuvi kupata maarifa mapya.

Amesema wavuvi watakaoshiriki ni wale wa bahari, maziwa na mabwawa yakiwemo ya Mtera na Nyumba ya Mungu.

Ameeleza kuwa mkutano huo utakuwa na midahalo ya kitaalamu itakayoleta matokeo ya tafiti za wataalamu wa vyuo vikuu ili kuleta chachu na kuwabadilisha mtazamo.

Pia, mkutano wa huo utakuwa na malengo ya kutoka na kauli moja kama Afrika yatakayowasilishwa katika mkutano kama huo katika ngazi ya  kimataifa utakaofanyika  Julai mwaka huu, nchini Italia ukiandaliwa na FAO.

"Tanzania tutaongoza msimamo wa Afrika kuhusu uvuvi mdogo na wavuvi wadogo ambao ndio wengi zaidi tutasema nini msimamo wetu, teknolojia, uwekezaji na kupata mitaji na uvuvi haramu.”

" Tanzania tutafungua fursa za uwekezaji zaidi kupitia sekta ya uvuvi na kufungua wigo wa mazao ya uvuvi na ufugaji samaki katika soko la nje," amesema.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Mei 23,2024 Msemaji wa wavuvi Tanzania,  Sijaona Kaloli amesema wanasubiri mwaliko kutoka wizara husika kuhusu mkutano huo, akisema ni muhimu kwa wavuvi kwani watapata fursa ya  kubadilishana maarifa  na wenzao wa mataifa mengine ya Afrika.