Diamond apata bima ya afya ya kwanza maishani mwake

Muktasari:

Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’ amesema katika maisha yake hajawahi kuwa na bima ya afya.

Msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’ amesema katika maisha yake hajawahi kuwa na bima ya afya.

Diamond ameyasema juzi alipokuwa akikabidhiwa kadi za bima ya afya za Resolution kwa ajili yake na watoto wake watatu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi hizo, Diamond amesema katika maisha yake hajawahi kuwa na bima ya afya.

Hata hivyo, amesema baada ya kupatiwa elimu na kampuni hiyo ya bima, ameona kuna umuhimu wa kuwa nayo ukizingatia kuwa yeye ni msanii anaweza kupata ajali hata akiwa kwenye jukwaa.

Kadi alizopewa kwaajili ya watoto wake Tiffah, Nillan na Dyllan, amesema zitampunguzia gharama ya matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa ResolutionInsurance, Marryanne Mugo, amesema bima hiyo mbali na kupata huduma za matibabu katika hospitali mbalimbali hapa nchini, pia itamwezesha Diamond kutibiwa nje ya nchi ikiwemo India na Uturuki endapo atapata rufaa za kimatibabu.

Wakati kwa upande wakazi wa Tandale, Mkurugenzi huyo amesema jumla ya kaya 250 zitapatiwa kadi hizo, na kila familia watoto wanne wataweza kutibiwa.

Alitaja thamani ya kadi hizo kuwa kila moja inagharimu Sh158,000 na wahusika watatakiwa kuzilipia kila mwaka.