Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Jafo awataka wananchi kulinda bwawa la Nyerere

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Selemani Jafo akiwa na baadhi ya wajumbe wa bodi ya Baraza la usimamizi wa mazingira (NEMC) walipofanya ziara ya kukagua utunzaji wa mazingira kwenye bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

Muktasari:

  • Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Selemani Jafo amewataka wananchi wanaoishi karibu na mito inayoingiza maji kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere kutunza mazingira ili mito hiyo isikauke.

Morogoro. Wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji vya mito inayoingiza maji kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere (JNHPP) wametakiwa kutunza mazingira ili vyanzo hivyo vya maji vizikauke.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Oktoba 4, 2023 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dk Selemani Jafo alipofanya ziara ya kukagua hali ya kimazingira kwenye ujenzi wa bwawa hilo.

Jafo amesema uzalishaji wa umeme kwenye bwawa hilo unategemea maji ya mito inayoingia Mto Rufiji ambapo ndipo lilipo Bwawa hilo hivyo wananchi wanaoishi kando ya mito hiyo watunze mazingira ili mito hiyo iendelee kupeleka maji kwenye bwawa hilo.

Ameitaja mito hiyo kuwa ni Mto Luwege, Mto Ruaha Mkuu na Mto Kilombero ambayo ndiyo chanzo cha maji kwenye uzalishaji wa nishati ya umeme kwenye bwawa hilo.

“Nimeelezwa hapa kuwa mradi huo umefikia asilimia 91 ya ujenzi na ukikamilika utasaidia kupunguza tatizo la nishati nchini hivyo ni lazima watu wanaoishi kwenye vyanzo vya maji kulinda mazingira ili vyanzo hivyo visikauke,” amesema Dk Jafo.

Amesema mradi huo ni wa Kimataifa hivyo suala la utunzaji wa mazingira ni lazima lizingatiwe ili watu kutoka nje waje wajifunze.

Dk Jafo amesema hali ya utunzaji wa mazingira katika mradi huo unaridhisha kwani wamefuatilia maeneo yote ya utupaji taka na maeneo ya kuchimba vifusi wameona kuwa yamezingatia viwango vya hali ya juu vya sheria ya mazingira

Amesema ujenzi wa bwawa umeendelea kujengwa kwa unadhifu wa hali ya juu kwa kuzingatia utii wa sheria na taratibu za kimazingira.

Naye mwenyekiti wa bodi ya Baraza la usimamizi wa mazingira (NEMC) Mhandisi, Esnat Chagu, amesema maeneo ambayo mito inayoleta maji kwenye bwawa la Julius Nyerere inatoka yanatakiwa kuangaliwa kwa umakini mkubwa katika utunzaji wa mazingira.

Amewataka watu wanaoishi kwenye vyanzo hivyo wawe watalii wa ndani kwa kuwa wa kwanza kwenda kuliona bwawa hilo ili waone umuhimu wa kutunza vyanzo hivyo ili visikauke.

Mhandisi Chagu amesema Nemc imeweka ofisi kwenye bwawa hilo kwa ajili ya kufuatilia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi huo na kufuatilia matatizo madogo madogo yanayojitokeza ili yasilete athari za kimazingira.

Ujenzi wa Bwawa la Julius Nyerere umegharimu Sh6.5 trilion huku likitarajiwa kuzalisha umeme Megawati 2,115 ambazo zinategemewa kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.