Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mollel atoa maelekezo Siku ya Hedhi Duniani

Muktasari:

  • Kufuatia maadhimisho ya siku ya hedhi salama Duniani mwaka 2023 kufanyika kwa Kongamano na maonyesho ya bidhaa za pedi kutoka kwa wadau mabalimbali, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema hataki kuona hilo likijirudia badala yake watoe elimu.

Dodoma. Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amesema hataki kuitwa kwenye ukumbi kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya hedhi salama Duniani ya mwaka 2024 kama ilivyofanywa mwaka huu, badala yake maaadhimisho hayo yafanyike kwa kutoa elimu ya hedhi salama na kugawa pedi kwa wenye uhitaji.

 Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya hedhi salama Duniani yaliyofanyika kitaifa Dodoma leo Mei 28, 2023, Dk Mollel amesema wazazi wengi wa maeneo ya vijijini hawana fedha na elimu kuhusu umuhimu wa kuwanunulia watoto wao pedi.

“Noamba mwaka kesho tujipange na hatutazungumza kuwa tumefanya utafiti au nini, tunataka tuzungumze tumegawa pedi shule ngapi, mashine ngapi ndio tunataka kusikia hiyo habari.

Na tunataka kukutana na nyie mtaani, nikija sitaki kuja kwenye ukumbi, nataka tukutane ‘site’ tena kule vijijini tukizindua hiyo mashine ya pedi, yani tusikutane ukumbini mjini,” amesema Dk Mollel.                                             

Juzi Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alizindua mashine yenye uwezo wa kuuza pisi moja ya pedi kwa Sh200 katika Shule ya Sekondari ya wasichana Bunge ikiwa na lengo la kumsaidia mwanafunzi kuendelea na masomo badala ya kukaa nyumbani kwenye siku zake za hedhi.

Hata hivyo kwa pamoja wadau waliofika kwenye maadhimisho hayo wamekubaliana ifikapo maadhimisho ya mwaka 2024 watakuwa wamekusanya pedi milioni 5 kwaajili ya kuzigawa sehemu zenye mahitaji.

Akizungumzia umuhimu wa kuwafikia wasichana sehemu za pembezoni, mdau wa hedhi kutoka mradi wa Femme International, Gladness Kampa amesema utoaji wa elimu utawasaidia wasichana kujihifadhi kwa njia salama na kuepuka magonjwa.