Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi: Uimara sera ya diplomasia kukuza uchumi Z'bar

Dk Mwinyi: Uimara sera ya diplomasia kukuza uchumi Z'bar

Muktasari:

  • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema ipo haja kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuimarisha sera ya diplomasia ya uchumi ili Zanzibar iweze kupata fursa zaidi katika kukuza uchumi wake.

Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema ipo haja kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuimarisha sera ya diplomasia ya uchumi ili Zanzibar iweze kupata fursa zaidi katika kukuza uchumi wake.


Dk Mwinyi ameyasema hayo leo Alhamisi Julai 29, 2021 Ikulu jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula


“Uchumi wa Zanzibar unategemea sana kazi zitakazofanywa na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania  nje ya nchi hasa ikizingatiwa kwamba Zanzibar ina bidhaa nyingi za kuuza nje ya nchi vikiwemo viungo,” amesema.


Amesema kwamba kwa kipindi kirefu Zanzibar imekuwa ikiingiza bidhaa nyingi kutoka nje ya nchi lakini haina bidhaa nyingi ambazo zinazotoka Zanzibar kwenda kuuzwa nje hivyo ni wakati sasa kuimarisha na sera ili bidhaa hizo ziweze kupata soko.


Alisema kuwa kuna nchi kadha zikiwemo zile za Jumuiya ya Nchi za Falme za Kiarabu (UAE), Oman na nchi nyinginezo zinahitaji bidhaa za Zanzibar hivyo, juhudi za makusudi zikichukuliwa mafanikio yanaweza kupatikana katika nyanja hiyo hasa ikizingatiwa kwamba fursa ipo.


Balozi Mulamula amesema ofisi za wizara yake zilizopo Zanzibar zimekuwa zikifanya kazi vizuri na kutoa ushirikiano mzuri kwa Serikali.


Pia amempongeza Dk Mwinyi kwa uwamuzi wake wa kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo imeleta mafanikio makubwa na imekuwa msaada kwa wizara yake katika kutekeleza majukumu yao.


“Kuwapo kwa maridhiano ya kisiasa hapa Zanzibar kumeweza kuwavutia watu wengi ambao wameonyesha nia ya kuja kufanya kazi hapa Zanzibar,” amesema.