Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Slaa afikishwa mahakamani akikabiliwa na shitaka moja

Balozi Mstaafu, Dk Wilbroad Silaa (katika) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Ijumaa Januari 10, 2025. Picha na Hadija Jumanne

Dar es Salaam. Mwanasiasa mkongwe, Wilbrod Slaa (76) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka moja la kusambaza taarifa za uongo katika mtandao wa X (zamani Twitter).

Dk Slaa amefikishwa mahakamani hapo leo Januari 10, 2025 na kusomewa kesi ya jinai namba 993 ya mwaka 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki.

Mapema leo Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alithibitisha kumshikilia Dk Slaa.

“Daktari yupo, tuko naye na tumekuwa na mahojiano naye kwa baadhi ya mambo na yanakwenda vizuri kwa hiyo tunaiangalia mifumo ya kisheria inatuelekeza ni nini cha kufanya na taarifa kamili zitatolewa baadaye,” amesema Kamanda Muliro.

Taarifa ya kukamatwa kwa Dk Slaa imesambaa kupitia mitandao ya kijamii, ikisikika sauti ya mwanasiasa huyo akizungumza kuhusu kukamatwa na Jeshi la Polisi na kwamba anapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Mbweni, Dar es Salaam.


Endelea kufuatilia Mwananchi.